Ticker

6/recent/ticker-posts

NEMC YASHIRIKI MAONESHO YA KWANZA YA UTALII YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Kushoto) wakiwa wanatoa maelezo kwa mgeni alietembelea banda la NEMC katika Maonesho ya kwanza ya Utalii ya Nchi za Afrika Mashariki yanayoendelea Jijijini Arusha.

Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira wakitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tumaini Senior walipotembelea banda la NEMC la maonesho ya kwanza ya utalii ya Nchi za Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Arusha.


***************************

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira linashiriki katika Maonesho ya kwanza ya Utalii ya nchi za Afrika Mashariki yaliyozinduliwa siku ya Jumamosi ya tarehe 9/10/2021 na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki. Kilele cha maonesho haya itakuwa tarehe 16/10/2021. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelenga kuyatumia katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii, bidhaa na huduma mbalimbali tunazozitoa katika sekta ya utalii.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetumia fursa ya maonesho haya kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira ikiwemo suala zima la umuhimu wa wawekezaji kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) kabla ya kuanzisha miradi katika sekta ya utalii.

Pia Baraza limepokea changamoto za kimazingira kutoka maeneo mbalimbali nchini hususani katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nyeti kiikolojia, usimamizi wa taka ngumu na kelele chafuzi.

Katika maonyesho haya ya kwanza ya utalii ya Nchi za Afrika Mashariki, takribani makampuni na mashirika/taasisi 155 yameshiriki. Pia vyombo vya habari mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi vimeshiriki.

Maonesho haya yametoa fursa kwa wadau mbalimbali katika sekta ya utalii na sekta nyingine wezeshi kukutana, kufahamiana na kubadilishana uzoefu katika uendeshaji na ukuzaji wa sekta ya utalii katika nchi zetu za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Baraza linapenda kutoa pongezi kwa waandaaji wa maonesho haya kwani yana tija na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini. Pia maonesho haya yanatoa fursa ya kupeana elimu juu ya uhifadhii endelevu wa vivutio vyetu vya utalii pamoja na mazingira kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments