Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATIMIZA NDOTO YA MEDICAL TOURISM ARUSHA



******************


Nteghenjwa Hosseah, Arusha

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa Sh. bilioni Moja kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, dharura, maabara, na huduma za dawa (OPD Complex) katika Hospital ya Jiji la Arusha.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali ya Halmashauri- ya Jiji la Arusha iliyopo eneo la Njiro, Rais Samia alisema fedha hizo zitazawezesha Jiji la Arusha kutimiza dhana ya huduma za matibabu ya Utalii (Medical Tourism) yenye lengo la kuinua utalii na kuifanya Jiji la Arusha kupata fedha za kigeni. 


Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amemhakilishia Mhe. Rais kuwa fedha hizo zitaletwa mara moja Katika Jiji la Arusha ili ziweze kufanya kazi hiyo kama alivyoelekeza.


Pia amewapongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuweza kujenga Hospitali hiyo ya Jiji kwa kutumia mapato ya ndani.


“Mhe Rais ujenzi wa hospitali hii mpaka hapa ilipofikia ni matunda ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, ule ushuru wanaotozwa wananchi, ada mbalimbali ndio zilizowezesha ujenzi wa hospitali hii, hongereni sana Jiji la Arusha kwa usimamizi mzuri wa mapato na kuelekeza kwenye miradi ya maendeleo."


Akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dkt.Maduhu Nindwa amesema mpaka sasa Sh bilioni 2.5 zimetumika katika ujenzi huo huku jengo la utawala likigharimu Sh milioni 535, jengo la mama na mtoto likitumia Sh 1.5 na ununuzi wa vifaa tiba na dawa Sh milioni 469.


Amesema Jengo la OPD Complex litakapokamilka litatoa huduma za kupokea wagonjwa wanaoletwa na helkopta ya wagonjwa haswa watalii, kuona na kupata ushauri wa Daktari, huduma za dharura, huduma za mionzi, huduma za dawa, kusafisha figo na damu, huduma ya mazoezi tiba ya viungo pamoja na huduma nyingine muhimu.




Dkt. Maduhu pia amebainisha kuwa baada ya jengo hilo kukamilika wataendelea kujenga jengo la nne ambalo litakua na huduma Jumuishi za upasuaji litakalotumika kutoa huduma za upasuaji za kibingwa na jengo la tano litajumiusha huduma jumuishi za utabibu wa ndani ili kukamilisha dhana ya Medical Tourism.

Post a Comment

0 Comments