Ticker

6/recent/ticker-posts

TAIFA STARS HOI, WACHAPWA BAO 1-0 NA BENIN KWENYE UWANJA WA MKAPA


*******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Taifa ya Benini katika mchezo wa makundi kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar.

Taifa Stars katika kipindi cha kwanza walicheza vizuri licha kupata nafasi nyingi za kufunga magoli walishindwa kuzitumia nafasi hizo na kuwafanya kwenda mapumziko kila timu haikupata kitu.

Kipindi cha pili timu ya Taifa ya Benini baada ya kufanya mabadiliko y wachezaji wao kadhaa ulizaa matunda kwani mchezo ulibadilika na kuanza kulisakama lango la timu ya Taifa ya Tanzania na baadae dakika ya 71 kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wao Steven Mounie kwa shuti kali ambalo lilimshinda Aishi Manula na kuingia nyavuni.

Juma lijalo timu hizo zitacheza mchezo mwingine ambapo Taifa Stars watawafuata Benin katika uwanja wao.

Post a Comment

0 Comments