Ticker

6/recent/ticker-posts

WINGI WA TWIGA KATIKA HIFADHI YA TAIFA NYERERE, YAWAVUTIA WATALII


Mmoja wa wanyama aina ya twiga akiwa katika malisho kwenye Hifadhi ya Taifa Nyerere. Baadhi ya Watalii wakiwasili katika uwanja wa Mtemere katika Hifadhi ya taifa Nyerere. Baadhi ya watalii wa kigeni wakipanda magari maalumu ya kuwatembeza watalii kwaajili ya kuangalia wanyama na maeneo mbalimbali ya kitalii katika Hifadhi ya Taifa NyerereMmoja wa wanyama aina ya twiga akiwa katika malisho kwenye Hifadhi ya Taifa Nyerere.

Baadhi ya watoto wa twiga ambao kwa kawaida hupenda kukaa kimakundi ambapo kitaalamu huitwa (nursery baby).Hupendelea kukaa kimakundi na kutafuta malisho japo kwa muda mwingine twiga wakubwa hukaa nao karibu kwasababu ya usalama.Twiga hawa wapo katika Hifadhi ya Taifa Nyerere.

Twiga akiwa karibu na mifereji ya maji ambayo hupeleka maji katika baadhi ya maziwa yaliyopo katika Hifadhi ya Taifa Nyerere.Katika hifadhi hii ya Nyerere kumekuwa na wimbi kubwa la twiga ambao pia wamekuwa vivutio vya watalii wanaokujja katika hifadhi hii. Kundi la Viboko wakiwa ndani ya maji katika moja ya ziwa lililopo katika Hifadhi ya Taifa Nyerere. Hifadhi hii pia inasifika kwa kuwa na Viboko wengi kuliko Hifadhi zote zilizopo nchini Tanzania. Mmoja wa wanyama aina ya Fisi akiwa katika Hifadhi ya Taifa Nyerere. Baadhi ya fisi wakiwa wamepumzika chini ya mti kwenye Hifadhi ya Taifa Nyerere (Nyerere National Park). Hifadhi hii pia inasifika kwa kuwa na wanyama haina ya Fisi kwenye maeneo tofautitofauti kwenye Hifadhi.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, NYERERE NATIONAL PARK

Licha yakuwa ni Hifadhi kubwa barani Afrika, Hifadhi ya Nyerere inasifika kwa kuwa na nyama wengi pia ikiwa ndiyo Hifadhi ambayo inaoongoza kwa kuwa na Twiga wengi.

Akizungumza katika hifadhi hiyo leo Mkurugenzi wa Kampuni ya Asilia, Bw.Brandon Kemp amesema hifadhi hiyo imekuwa ikipendwa na watalii wengi hivyo kumekuwa na watalii mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi wamekuwa wakifika katika hifadhi hiyo kwaajili ya kutalii

"Tumekuwa tukishirikiana kwa karibu na TANAPA kuhakikisha watalii wanafika hapa na kupata huduma stahiki ambazo anapaswa kupatiwa na baadae wanaitangaza kwa mazuri hifadhi hiyo". Amesema Bw.Kemp

Kwa upande wake Muongoza Watalii, Bw.Felix Mpelembwa amesema kumekuwa na wimbi kubwa la swala katika hifadhi hiyo hasa katika kipindi hiki cha mwezi Septemba na Oktoba kwasababu ndicho kipondi ambacho swala huzaliana.

Amesema hifadhi hiyo imekuwa ikisifika pia kuwa na Viboko na mambo wa kutosha katika maziwa ambayo yamo ndani ya hifadhi hiyo na kufanya watalii wengi kupendelea kufika katika hifadhi hiyo.

Post a Comment

0 Comments