Ticker

6/recent/ticker-posts

ASTON VILLA YAMTANGAZA GERRARD KUWA KOCHA WAO MKUU


********************* 

NA EMMANUEL MBATILO 

Klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza imemtangaza Steven Gerrard kuwa kocha wao Mkuu kuchukua mikoba ya Dean Smith ambaye alitimuliwa hivi karibuni kutokana na matokeo mabovu. 

Gerrard alikuwa mchezaji wa Liverpool kwa muda mrefu na kupata mafanikio makubwa kwenye klabu hiyo na baadae kustaafu kucheza soka. 

Mwaka 2018 Steven Gerrard alitangazwa kuwa kocha Mkuu wa klabu ya Rangers ya nchini Scotland ambapo kwenye hiyo ameipa mafanikio ikiwemo kushinda taji la ligi hiyo.

Post a Comment

0 Comments