Ticker

6/recent/ticker-posts

BODI YA WABUNIFU WA MAJENGO KUWAFUNDA WATALAMU WA UNJENZI



******************************

Na Richard Mrusha

Bodi ya Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi( AQRB) imeishauri jamii kutumia wataalamu wa ujenzi waliosajiliwa ili kusaidia miradi ya ujenzi kudumu kwa muda mrefu nakwamba hali hiyo inasaidia kupunguza gharama za ujenzi .

Ushauri huo umetolewa na Mbunifu Majengo Arch.Msajiri wa Bodi hiyo Edwini Nnunduma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mafunzo endelevu ya CPD yatakayofanyika mkoani Mwanza Desemba 2 na 3 Mwaka huu huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel Robaert.

Arch.Nnunduma amesema kwamba baadhi ya Jamii imekua ikitumia mafundi waliosomea katika vyuo vya ufundi mbalimbali kama vile VETA katika kufanya shughuli za ujenzi bila kutumia wataalamu wa ujenzi waliosajiriwa na bodi hiyo hali ambayo amesema inachangia majengo mengi kutokua na ubora.

“Sisi tunasisitiza wataalamu wetu watumike hata katika kazi binafsi,inasaidia kufahamu ghamara za ujenzi kabla ujenzi hujaanza kufanyika,lakini pia inasaidia kujenga nyumba zenye ubora kulingana na uwezo wa mtu kiuchumi”amesema ARCH.Mnunduma.

Kuhusu semina ya mafunzo endelevu Nnunduma amesema kwamba Semina hiuo inatarajiwa kuwa na washiriki wapatao 250 hadi 300 ambao ni wataalamu katika sekta tofauti ikiwemo Wabunifu wa Majengo,Wakadiriaji wa Majenzi,Wasimamizi wa Majengo,Wasimamizi wa Miradi na Wasamabazaji wa Vifaa vya Ujenzi.

Aidha amesema kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ,ikiwemo mada kuhusu sheria mpya ya Kodi kwenye Sekta ya Ujenzi ambapo wataalamu hao watafundishwa namna ya kupeleka mapato TRA kwa njia ya kielektroniki kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia na kisayansi.

Post a Comment

0 Comments