Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi.

******************************

Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuendelea kufanya mageuzi ya kiuongozi na kiutendaji ili kukidhi mahitaji ya wakati, mwenendo wa mabadiliko ya siasa za dunia na madhumuni ya Chama chetu katika kuwatumikia wananchi kikamilifu.

Hivyo Chama kimefanya uteuzi wa makatibu wa mikoa 32, waliobaki vituo vyao vya kazi ni 10, waliopangiwa vituo vipya ni 12 na wapya ni 9; aidha makatibu wa wilaya ni 168 ambapo waliopangiwa vituo vipya ni 67, waliobaki kwenye vituo vyao vya kazi ni 45 na wapya ni 56. Katika uteuzi huu kwa kuzingatia suala la jinsia wanawake ni 67 sawa na asilimia 33.5 na wanaume ni 133 sawa na asilimia 66.5.

Katika uteuzi huu hakuna hata mmoja aliyetoka nje ya mfumo wa Chama Cha Mapinduzi. Makatibu wapya wa Mikoa na Wilaya wametokana na kupandishwa hadhi kwa makatibu wa CCM wa Wilaya, makatibu wa jumuiya za CCM Wilaya na Mikoa, Maafisa wa Chama na jumuiya Makao Makuu kwa utendaji kazi wao mzuri pamoja na makatibu waliorejeshwa kwenye utumishi kutokana na utiifu wao kwa Chama.

Katika uteuzi huu Kamati kuu ya Halmashauri kuu ilizingatia sifa za ziada ikiwemo uadilifu, uaminifu, weledi, uwezo, bidii, ubunifu, jinsia na rika. Makatibu wapya na waliohamishwa vituo vya kazi kwa Mikoa na Wilaya wanatakiwa kuripoti vituo vyao vya kazi mara baada ya kupokea barua zao. Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa na Wilaya uliofanyika ni kama ifuatavyo:-

Uteuzi huu umeanza mara moja kuanzia tarehe 6 Novemba, 2021.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,
Itikadi na Uenezi.
8 Novemba,2021
 

A.  MAKATIBU WA CCM WA MKOA

Na

Jina Kamili

KITUO

1

Ndg. Mussa Dadi Matoroka

Arusha

2

Ndg. Adam Ngalawa

 Dar Es Salaam

3

Ndg. Pili Mbanga

Dodoma

4

Ndg. Mwanamasudi Pazi

Rukwa

5

Ndg. Naomi Kapambala

Manyara

6

Ndg.Omar Mtuwa

 Katavi

7

Ndg. Rukia Mkindu

Iringa

8

Ndg. Innocent Nanzabar

Simiyu

9

Ndg. Elias Mpanda

Morogoro

10

Ndg. Marco Mbanga

Kaskazini Pemba

11

Alhaji Saad Kusilawe

 Mbeya

12

Ndg. Donald Etamya Magesa

Shinyanga

13

Ndg. Yusuf Said Goha

 Pwani

14

Ndg.  Barnabas Essau

Lindi

15

Ndg. Langael Akyoo

Mara

16

Ndg. Alexandrina Katabi

Geita

17

Ndg. Suleiman Mzee

Tanga

18

Ndg. Mobutu Malima

Kigoma

19

Ndg. Julius Peter

Mwanza

20

Ndg. Christopher Palangyo

Kagera

21

Ndg. Mgeni Musa Haji

 Mtwara

22

Ndg. Lucy B. Shee

Singida

23

Ndg. Solomon Kasaba

Tabora

24

Ndg. Jonathan Mabihya

Kilimanjaro

25

Ndg. Mullar Othuman Zuber

Magharibi

26

Ndg. Mohamed Ally  Khalfan

Kusini Pemba

27

Ndg. Shaibu Akwilombe

Ruvuma

28

Ndg. Amina Imbo

Kusini Unguja

29

Ndg. Abdullar Mwinyi Hassan

Njombe

30

Ndg. Salum Suleiman Tate

Mjini

31

Ndg. Juma Mpeli

Songwe

32

Ndg. Ramadhan Rajab (Kapeto)

Kaskazini Unguja

 

B.  MAKATIBU WA CCM WA WILAYA

1. ARUSHA

...

NA

JINA KAMILI

KITUO

1.  

Ndg. Kataba Sukuru

Arusha Mjini

2.  

Ndg. Shaban Mrisho

Karatu

3.  

Ndg. Safina Alfred

Monduli

4.  

Ndg. Aboubakar Ghaty

Ngorongoro

5.  

Ndg. Mwadawa Maulid

ArumeruPost a Comment

0 Comments