Ticker

6/recent/ticker-posts

DC HANANG' AONGOZA SHUGHULI MBALIMBALI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU

Mkuu wa Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, Janeth Mayanja akipanda mti ikiwa ni moja ya shughuli zilizofanyika katika Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 60 ya Uhuru yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Katesh.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, Janeth Mayanja akiwa na viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo..
Vijana wakiwa tayari kwa kuanza ziadha kwenye maadhimisho hayo
Riadha ikiwa imeanza.
Mchezo wa kukimbiza kuku ukifanyika
Mshindi wa kukimbiza kuku akiwa na kuku wake mbele ya viongozi waliokuwepo kwenye maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe ziwa zimebamba.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hizo.


Na Dotto Mwaibale, Hanang'
WILAYA ya Hanang' imefanya kumbukizi ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya shughuli mbalimbali Ikiwemo kupanda miti, mchezo wa kufukuza kuku, mashindano ya Riadha pamoja na maonyesho ya ujasiriamali.

Akizungumza katika kumbukizi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano Ili kunufaika na Uhuru wa nchi yetu.

Mayanja alitumia nafasi hiyo kuishukuru kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo, viongozi wastaafu,viongozi wote wa wilaya, wadau mbalimbali pamoja na wananchi kwa kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho hayo.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja Vya Shule ya Msingi Katesh, wilayani humo mkoani Manyara.

Post a Comment

0 Comments