Ticker

6/recent/ticker-posts

MADIWANI IKUNGI WAPITISHA AZIMIO LA KUMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliketi juzi na kupitisha azimio la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kutoa fedha za miradi katika halmashauri hiyo. Kushoto ni Mgeni rasmi wa kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro.

Kikao kikiendelea.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao hicho kikiendelea.
Madiwani wakipitia taarifa mbalimbali katika kikao hicho.
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakiwa meza kuu wakati wa kikao hicho.

*********************
Na Dotto Mwaibale, Singida

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya ikungi mkoani Singida katika kikao cha kawida cha baraza hilo kilichofanyika jana wamepitisha kwa kauli moja azimio kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia halmashauri hiyo kupewa zaidi ya Sh. 3 Bilioni ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotolewa katika kupambana na Changamoto za UVIKO 19.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ally Mwanga akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza hilo alisema halmashauri imepokea ya Sh. 2.6 Bilioni fedha za ujenzi wa madarasa 67 mapya ya shule za sekondari na madarasa 65 mapya ya shule shikizi za msingi na zaidi ya milioni 860 kwenye miradi ya maji.

Mwanga alisema fedha hizo ni nyingi ambazo zilikuwa nje ya bajeti ya Halmashauri na kwa pamoja wamemuomba Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao hicho kufikisha salamu na azimio la pongezi la madiwani kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa kupokea azimio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro alisema Serikali itaendelea kupeleka fedha za miradi ya maendeleo kama ambavyo imelekezwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusisitiza kuwa itaendelea kutafuta vyanzo vipya vya fedha kwa ajili ya kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za kijamii.

Post a Comment

0 Comments