Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA NAMNA ALIVYOIBEBA AGENDA YA USHIRIKISHWAJI WA SEKTA BINAFASI


MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye studio za kituo cha TV cha Azam TV

***********************

NA MWANDISHI WETU, DAR.

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za KIraia Tanzania Bara NGOs Neema Lugangira amemshukuru Rais Samila Suluhu kwa namna alivyoibeba agenda ya Local Content na Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi


Mbunge Lugangira aliyasema hayo leo asubuhi wakati wa kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na kituo cha luninga cha Azam TV ambapo kubwa zaidi walikuwa wakijadili kuhusu Fursa za Vijana katika Ujenzi wa Bomba la Mafuta la Uganda-Tanzania.


Akiwa kwenye kipindi hicho Mbunge Neema Lugangira alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa kuweka mazingira Wezeshi ya Watanzania kushiriki katika fursa za Sekta ya Uziduaji; Madini, Mafuta na Gesi Asilia


Aidha amewakumbusha Vijana kufika Ofisi za Serikali za Mitaa, Ofisi za TPDC, EWURA, na TPSF ili Vijana wazijue fursa na wanaweza kushiriki vipi


Huku akirejea ushauri aliowahi kutoa kwa EWURA kuboresha Vigezo vya Usajili katika Kanzi Data. Mfano, kwa Vigezo vya sasa NGOs haziwezi kujisajili na Kundi la Wajasiriamali kama Mama Lishe, Wakulima, Wafugaji n.k. pia hawawezi kujisajili.


Alisisitiza pia umuhimu wa Taasisi ya Sekta Binafsi TZ yaani TPSF kushirikiana na NGOs za Vijana na kuandaa Makongamano Mahsusi kwa Kujadili kwa Kina juu ya Fursa za Vijana na kuweka Mpango Mkakati wa Kuanzisha Enterprise Development Centre #EDC


Hata hivyo Mbunge Neema alisema ni muhimu suala la Uwazi wa Fursa za Vijana na Wananchi wanaotoka Mikoa 8, Wilaya 24, Vijiji 226 ambapo Bomba la Mafuta Uganda-Tanzania linapita ambao ndio Jamii itakayoishi na kulinda Mradi na Unufaikaji wa Jamii hii Utaimarisha Usalama wa Mradi.

Post a Comment

0 Comments