Ticker

6/recent/ticker-posts

MARY MASANJA ATEMBELEA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA KUHIMIZA KUTANGAZA UTALII


Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo akimkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja alipotembelea Ofisi za Ubalozi mapema leo. Mhe. Masanja yupo nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Uongozi wa Utalii Afrika na Tuzo za Wiki ya Kusafiri litakalofanyika kesho kwenye hoteli ya Kigali Serena.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akisalimiana na watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda alipotembelea Ofisi za Ubalozi mapema leo. Mhe. Masanja yupo nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Uongozi wa Utalii Afrika na Tuzo za Wiki ya Kusafiri litakalofanyika kesho kwenye hoteli ya Kigali Serena.


Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (kulia) akichangia mada kuhusu mikakati ya kukuza utalii wa Tanzania alipotembelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) ofisini kwake leo. Wengine ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, Happiness Ruangisa (wa pili kutoka kulia) na Mwambata wa Jeshi, Kanali Ramadhan Dogoli (wa tatu kutoka kulia)wakifuatilia mada.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akitoa maelekezo ya namna ya kukuza utalii kupitia balozi za Tanzania, alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda mapema leo. Wengine ni Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (kulia), Mkuu wa Fedha na Utawala, Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, Happiness Ruangisa (wa pili kutoka kulia) na Mwambata wa Jeshi, Kanali Ramadhan Dogoli (wa tatu kutoka kulia) wakifuatilia mada


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu maboresho yaliyofanyika ya kuendeleza utalii nchini Tanzania wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (hayupo pichani) na Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (hayupo pichani).


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda mara baada ya kikao kilichofanyika mapema leo. Wengine ni Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (wa nne kutoka kulia) na Mkurugenzi Idara ya Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga (wa pili kutoka kushoto).

Post a Comment

0 Comments