Ticker

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA OMUKA HUB LAANZISHA PROGRAMU KWA KUSHIRIKIANA NA WABUNGE KUPINGA UKATILII WA KIJINSIA MITANDAONI KWA WANAWAKE WANASIASA






*******
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM


Shirika la Omuka Hub iliyoanzishwa na Mhe Neema Lugangira kwa lengo la kuimarisha ushiriki wa sekta ya kidijitali kwa vijana, wanawake, wanahabri, shule na usalama wa intaneti kwa mikoa iliyo pembezoni mwa Tanzania.


Moja ya Vipaumbele vya Omuka Hub ni kuhakikisha kunawepo mazingira wezeshi ya kuwafanya Wanawake Wanasiasa kuwa salama wanapokuwa Mitandaoni hivyo kuanzisha Programu ya Kupinga Ukatilii wa Kijinsia Mitandaoni kwa Wanawake Wanasiasa.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Omuka Hub, Lovelet Lwakatare, wakati wa Maonyesho ya Teknologia ya Kupambana na Ukatili wa Kijinsia yaliyoandaliwa na Shirika la Tangible Tanzania ambalo Mkurugenzi wake ni Madam Geline Fuko.


“Kwa upande wa Ukatili wa Kijinsia, sisi Omuka Hub tumejikita zaidi katika kupambana na ukatili wa kijinsia mitandaoni wanaofanyiwa wanawake wanasiasa na kupitia programu yetu hii tumeanzisha Kikundi cha Wabunge Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake Wanasiasa.

Kikundi hiki kina Wabunge 21 Vinara kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua kushirikiana kupaza sauti kupinga ukatili wa aina hii na kupitia Programu yetu tutahakikisha tunaweza mazingira wezeshi ya usalama mitandaoni kupitia maboresho wa Sera, Sheria na Kanuni.” Alisema Lovelet.

Aidha aliongeza kuwa uzoefu mitandaoni unatuonyesha kwamba wanawake wanasiasa wanavyokuwa katika mitandao ya kijamii na wakiweka kazi zao, kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajikiti katika hoja kwa kuchangia au kuuliza maswali bali wanahamishia hoja upande wa uanamke wao kama muonekano wao, jambo ambalo halifanyiki kwa wanaume wanasiasa.

"Shirika la Omuka Hub linapinga ukatili huo na tunataka tuchangie kuweka usawa wa kijinsia mitandaoni ili mwanamke mwanasiasa aweze kutumia Mitandao kwa uhuru sawa na makundi mengine.

Hii itasaidia wanawake waweze kujiamini wanapokuwa katika mitandao ya kijamii kuzungumza na wananchi wao bila kuulizwa kwa nini nywele amekata, kwanini amevaa vile ambavyo amevaa, anafaa kwa hili, kwa lile na hivyo ndivyo ambavyo tutawawezesha wanawake wengi zaidi kushiriki kwenye siasa na kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa.

Katika maadhimisho hayo ya siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia duniani kote ambayo dunia inajitambulisha kama The ‘Orange World’ “Sisi Omuka Hub tunapinga, tunakemea tunatoa rai kwa watu wote kuacha ukatili wa kijinsia wanaofanya mitandaoni kwa wanawake wanasiasa na tunahamasisha watu wanapokuwa katika mijadala waweze kuchangia kwa hoja na isiwe muonekano wao, mavazi yao, familia zao au masuala yao binafsi." Alisema Lovelet.

"Kwa niaba ya Omuka Hub tunamshukuru sana Madam Geline Fuko, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tangible Tanzania kwa kutupa fursa ya kuwa kati ya Mashirika yaliyochaguliwa kushiriki katika maonyesho ya teknologia ya kupambana na ukatili wa kijinsia katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl Nyerere Dar es Salaam, tarehe 26 Novemba 2021 na tulifurahia sana mrejesho mazuri ya kazi zetu tuliopata kutoka kwa Mgeni Rasmi, Mhe Madam Kate Somvongsiri, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Serikali ya Marekani (USAID Mission Director, Tanzania). " alimalizia Lovelet.


Wabunge 21 ambao ni Wabunge Vinara wa Kupinga Ukatilii wa Kijinsia Mitandaoni kwa Wanawake Wanasiasa (MP Champions Addressing Online Gender Based Violence on Women in Politics) ni Neema Lugangira, Salome Makamba, Nusrat Hanje, Judith Kapinga, Felista Njau, Condester Sichalwe, Ng'wasi Kamani, Jesca Kishoa, Keysha Khadija Taya, Tauhida Garlos, Mariam Ditopile, Catherine Magige, Lathifa Juakali, Rashid Shangazi, Elly Kingu, Abubakari Assenga, Festo Sanga, Rama S. Rama, Zaytuni Swai, Kassim Hassan Haji na Jacqueline Msongozi.

Post a Comment

0 Comments