Ticker

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WATAKIWA KUHIFADHI MATUMIZI ENDELEVU YA MALIKALE NCHINI.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akiwaeleza wadau wa Malikale mipango mikakati ya Makumbusho.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga (kulia),Muhifadhi Mkuu wa Mambo ya Kale kutoka wizara ya Maliasil na Utalii Mwita William (katikati) wakimsikiliza mdau wa Malikale Profesa Adolfo Mascarepha.
Mkuu wa Kitengo cha Malikale Makumbusho ya Taifa Revocatus Bugumba akizungumza katika warsha hiyo.
Afisa utamaduni kutoka Manispaa ya Ubungo Ritha Nguruwe akizungumza na wanahabari kueleza namna kama Manispaa watakavyokwenda kutekeleza mikakati waliojiwekea katika uhifadhi wa MalikaleMkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga (katikati mwenye suti ya bluu) kwenye picha ya pamoja wadau wa Malikale


.................................


NA MUSSA KHALID.

Shirika la Makumbusho ya Taifa Nchini limeanda mpango mkakati wa kuwahamasisha wadau wa uhifadhi na serikali za mitaa 50 kushiriki katika kuhifadhi na matumizi endelevu wa malikale kwa kipindi cha miaka mitano 2021-2016 ili kuvutia watalii kutembelea maeneo hayo.

Hayo yameelezwa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akizungumza kwenye warsha iliyowakutanisha wadau mbalimbali nchini yenye lengo la kujadili namna ya utekelezaji wa sera za uhifadhi Malikale ili ziweze kuwanufaisha jamii husika wa eneo Hilo.

Dkt Lwoga amesema kuwa watahakikisha wanaandaa na kuendesha Program 240 za kuhamasisha jamii kuufahamu na kutembelea utalii wa kiutamaduni.

"Sera ya Malikale ya Mwaka 2008 na sheria ya Mambo ya Kale sura 333 inatoa nafasi kwa wadau kushiriki kwenye Shughuli za uhifadhi na uendelezaji wa mali kale hivyo Malengo yetu pia ni kuweka mikakati mbalimbali ya uhifadhi WA maeneo ya Malikale za Dar es salaam kwa kushirikiana baina ya wadau wa Makumbusho ya Taifa"amesema Dkt Lwoga

Aidha Mkurugenzi huyo ameeleza pia mipango ya ni kuanzisha na kusimamia mashirikiano ya kitaifa kikanda na Kimataifa katika nyanja za uhifadhi,utafiti, maonyesho pamoja na program.

Awali akizungumza Muhifadhi Mkuu wa Mambo ya Kale kutoka wizara ya Maliasili na Utalii Mwita William amewataka wa Tanzania kutumia fursa zilizopo Katika sekta ya Malikale ili waweze kuzitumia kwenye Jamii na kiuchumi jambo litakalosaidia kuwavutia watalii na hivyo serikali kunufaika kwa kuongeza Fedha za kigeni.

"Ni washauri watanzania kutumia fursa mbalimbali kwani sera zinaruhusu watu kuanzisha matamasha ya Kumbukumbu za kihistoria ambapo wanaweza pia kujiajiri"amesema William

Naye Afisa utamaduni kutoka Manispaa ya Ubungo Ritha Nguruwe amesema kuwa wamepata uelewa wa kwenda kuzitambua na kupanga namna ya kuzihifadhi Malikake lakini pia kutoa Elimu kwa wananchi kwani baadhi hawana uelewa wa kuzitunza Malikale.

Kwa upande wao baadhi ya wadau akiwemo Mhadhiri Mwandamizi Idara ya Ikolojia na Mkurugenzi wa Utafiti Katika Ndaki ya Hisia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt Pastory Magayane,Muongoza utalii kutoka Taasisi ya Tourguide Association Tetula Okama pamoja na mdau Profesa Adolfo Mascarepha wamesema ni vyema Elimu ikaendelea kutolewa ili Watanzania waweze kuufahamu jinsi ya kuweza kuzitunza na kuhifadhi Malikale katika maeneo yao.

Hata hivyo Makumbusho hiyo imepanga kuendelea kuwahamasisha watu mbalimbali kutembelea maeneo ya Malikale Kwa kuandaa mpango wa masoko kuchapisha vipeperushi,kuandika makala simulizi na kuandaa vipindi mbalimbali kwa vyombo vya Habari.

Post a Comment

0 Comments