Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY: TARAJIENI MAKUBWA UJENZI BARABARA VIJIJINI**************************

Na Angela Msimbira, Mwanga


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu amesema dhamira ya dhati ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha inajenga miundombinu ya barabara maeneo ya vijijini kwa kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara maeneo ya vijijini kupitia wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA)

Akikagua ujenzi wa barabara ya Kisangara - Shighatini na kifula - Butu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Leo Waziri Ummy amesema bajeti ya Tarura katika Halmashauri hiyo imeongezeka kutoka shilingi milioni 695 kwa mwaka wa fedha 2020 hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 kwa mwaka wa fedha 2021

Amesema kuwa wananchi wategemee mabadiliko makubwa katika suala zima la ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ya vijijini lengo likiwa ni kuwapunguzia adha wananchi na kufungua uchumi wa wakazi wa Mwaga kwa kuwa barabara nyingi zitafunguliwa,Amemuagiza Mkandarasi anayejenga barabara hiyo Elerai Construction Co Limited kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa barabara hizo kwa wakati kwa kuhakikisha wanafuata viwango vilivyowekwa na Serikali

Aidha, ujenzi wa barabara ya Kisangara - Shighatini (km3. 57) na Kifula - Butu (km 3.57) itajengwa kwa kiwango cha lami na itagharimu zaidi ya shilingi milioni 441.


Post a Comment

0 Comments