Ticker

6/recent/ticker-posts

WCF YAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA UTUMISHI/UTAWALA KUTOKA TAMISEMI

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

MAAFISA Utumishi/Utawala kote nchini wamehimizwa kujenga mahusiano baina ya ofisi zao na Wafanyakazi katika kulinda haki zao ikiwa ni pamoja na kufahamu masuala yahusuyo fidia baada ya mfanyakazi kuumia au kuugua kutokana na kazi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma mjini Morogoro Jumatatu Novemba 22, 2021 kwenye kikao kazi cha kuwajengea uwezo maafisa hao walio chini ya TAMISEMI kuelewa huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

Alisema jumla ya washiriki 100 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Singida na Dodoma pamoja na kujifunza kuhusu usalama mahali pa kazi, pia wamejifunza namna ya kuwasilisha madai pindi mfanyakazi anapoumia kutokana na ajali, kuugua au kifo kinachotokana na kazi.

“Dhumuni kubwa la mafunzo haya ni kuwapa uelewa kuhusu , huduma zitolewazo na mfuko na hatua za kufuata wakati wa kuwasilisha madai hususan kuwasilisha madai kwa njia ya mtandao (Online Notification System-ONS) inayopatikana kwenye portal.wcf.go.tz na masuala ya Usalama na Afya mahala pa kazi” Alifafanua Dkt. Mduma.

Dkt. Mduma alisema Dhamira ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa na uchumi endelevu ambao utahakikisha Tanzania kubaki katika kundi la nchi zenye uchumi wa wa kati kisha kupanda kwenye uchumi wa juu zaidi.

“Dhamira hii itawezekana pale ambapo tutakuwa na wafanyakazi wenye uhakika wa usalama wa afya zao katika maeneo yao ya kazi na endapo itatokea bahati mbaya wakapata madhara wakiwa wanafanya kazi basi wawe na uhakika wa kupata fidia stahiki na kwa wakati.” Alisema.

Awali Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar alisema, mafunzo haya ni ya kwanza kwa kundi la Maafisa kutoka TAMISEMI na yatakuwa endelevu.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo mmoja wa washiriki Bw. Khamisi Khatib Khamisi ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Mafya mkoani Pwani, alisema yamewasaidia sana kuwajengea uwezo wa kujua ni hatua gani za kufuata endapo mfanyakazi ataumia au kuugua kutokana na kazi anazozifanya.

“Na mimi nitakapotoka hapa nitashauriana na wenzangu ili tuwapatie elimu watumishi wetu wilayani ili nao watambue kuwa WCF iko kwa ajili yao na endapo watapata madhara yoyote yatokanayo na kazi iwe rahisi kwao kufuata taratibu zitakazowezesha kupata haki zao kutoka WCF.” Alisema Khamisi.

Washiriki hao pia walijifunza aina za Mafao ya Fidia yanayotolewa na WCF kwa Mfanyakazi aliyeumia, kuugua kutokana na kazi na wategemezi wa mfanyaakzi aliyefariki kutokana na kazi.

Hali kadhalika walipata fursa ya kuona kwa onyesho la hatua za kuchukua endapo mfanyakazi atapata ajali akiwa kazini, namna ya kuwasilisha madai kwa njia ya mtandao.Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, akiwahutubia Maafisa Utumishi/Utawala kutoka TAMISEMI wakati wa semina ya kuwajengea uwezo kuhusu Afya na Usalama mahala pa kazi na shughuliza Mfuko mjini Morogoro Novemba 22, 2021. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (kushoto) na Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar wakifurahia jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akitoa elimu kwa washiriki.
Washiriki wakifuatilia mafunzo
Washiriki wakifuatilia mafunzo
Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi, akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki kufuatia mada aliyotoa ya Usalama na Afya mahali pa Kazi.
Afisa Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi WCF, Bw. Robert Duguza akitoa mada kuhusu namna ya kuwasilisha madai ya fidia ambapo alisema sheria inasema unapaswa kuwasilisha taarifa hiyo walau ndani ya miezi 12 tangu ajali ilipotokea na inapozidi miezi 12 taarifa haijatolewa mfanyakazi anakuwa amepoteza haki ya kudai fidia WCF.
Mmoja wa washiriki akizungumza
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Mmoja wa washiriki akipitia kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za WCF
Bi. Tumaini Kyano kutoka WCF akipanga makabrasha yaliyotumiwa na washiriki.
Bi. Amina Likuvungwa, Afisa Madai Mkuu, WCF akiweka sawa makabrasha muda mfupi kabla ya mafunzo kuanza
Mshiriki akijisajili mbele ya Afisa wa WCF,
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge akiongoza mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi, akiwasilisha mada kuhusu Afya na Usalama mahali pa kazi.

Post a Comment

0 Comments