AFISA Misitu Mkuu Emanuel Msofe akizungumza wakati wa warsha ya kutambulisha mradi wa FORVAC kwa viongozi wapya walioteliwa hivi karibuni iliyofanyika Jijini Tanga ambapo alisema kwa sasa zipo njia mbalimbali zinafanyika kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua warsha hiyo
Meneja wa Mradi wa Forvac kwa upande wa Makao makuu Dodoma Alex Njahani akizungumza na waandishi wa habari
KATIBU Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta katikati akiwa na washiriki wengine kwenye warsha hiyo
*********************
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
AFISA Misitu Mkuu Emanuel Msofe amesema takwimu zinaonyesha zaidi ya hekta 469,000 za misitu zinapotea kila mwaka na kama hakutakuwa na njia mbalimbali za kudhibiti uharibifu wa misitu inaweza kupelekea vizazi vijavyo vikakosa kufaidi rasilimali hiyo ya misitu.
Msofe ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliyasema hayo leo wakati wa warsha ya kutambulisha mradi wa FORVAC kwa viongozi wapya walioteliwa hivi karibuni iliyofanyika Jijini Tanga ambapo alisema kwa sasa zipo njia mbalimbali zinafanyika.
Alisema njia hizo ni kutumia lazima kuwepo lakini kutumia huko kuwe kunatokana na mpango ulioandaliwa wa uvunaji wa misitu uwe endelevu ambao kupitia mpango huo msitu ambapo unavunwa eneo dogo la msitu kama asilimia 10 na nyengine linabaki kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu.
Aidha aliongeza pia ikiwemo vyanzo vya maji na maeneo mbalimbali ambao wanyama wanaishi na kuzaliana
Afisa Misitu huyo alisema idara ya misitu na nyuki iliyo chini ya wizara ya maliasiali na utalii inashughulika kuandaa sera sheria ,kanuni na miongozo mbalimbali ya kusimamia misitu kiundelevu hapa Tanzania.
“ Kama mliovyoona programa ya Forvac ni matunda ya program zilizo kwenye mpango wa idara ya misitu na nyuki sasa mnavyojua ni kwamba misitu ipo kwa ajili ya mambo mbalimbali kwanza mifumo ya ikilojia kuhakikisha kuwa kunakuwa na mvua na hewa safi “Alisema
Alisema lakini pia kunakuwa na mazingira wezeshi kwa wanyama ambao wanategemea pamoja na binadamu kutokana na kwamba zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wanatumia nishati ya kuni mkaa kwa ajili ya kupata huduma ya nishati majumbani.
“Lakini mito mingi zaidi ya asilimia 50 inatoka kwenye misitu maana yake misitu ndio inahifadhi maji sasa changamoto kunakuwa na matumizi ambayo sio endelevu yanachangia kupungua kwa misitu na sasa “Alisema
Awali akizungumza wakati akifungua warsha hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema wanashukuru na kupongeza Forvac kwa mradi mzuri ambao wanaendelea kuufanya kwao maanake wanakwenda kuvijengea uwezo vijiji ili viweze kuona umuhimu wa kutunza rasilimali misitu.
Alisema pamoja na hayo ni kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao yanayotokana na misitu na kama wanavyojua kadiri dunia inayokwenda wanakumbana na mabadiliko ya tabia ya nchi kana kwamba hali ya hewa haitabiriki baadhi ya viumbe hai navyo nyengine vimekuwa vikipotea.
Naye kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Forvac kwa upande wa Makao makuu Dodoma Alex Njahani alisema mradi huo ni wa miaka minne na mwakani mwezi wa saba utafika mwisho kwa hiyo kipindi cha miaka mitatu na zaidi tayari wanacha kujivunia kama mradi wamevifanya ambavyo vinaonekana.
Alisema lengo la mradi lilikuwa ni kuongeza thamani mazao ya misitu na tayari kuna kazi zimefanyika na kwa mfano kwenye mkoa wa Tanga wilaya ya Kilindi na Handeni vile vijiji vimeanza kuvuna hivyo tayari mnyororo wa mazao maana yake umeanza. Meneja huyo alisema pia asali ni mnoyoyo ambao unajitegemea na wamekwenda hatua nzuri na wilaya ya Handeni tayari wamesaidia mizinga ya nyuki zaidi ya 50 na vifaa nyengine vya milioni 98 mwezi Julai mwaka huu na tayari wameanza kuvuna asali tani 1.5 kutokana na mizinga waliowezesha hilo wanajivunia kama mradi .
0 Comments