Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YAICHAPA RUVU SHOOTING MABAO 3-1 CCM KIRUMBA MWANZA


**************


NA EMMANUEL MBATILO 


Klabu ya Simba imefanikiwa kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi ya NBC ukiochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mechi ilikuwa ya aina yake ambapo kocha mpya wa Simba Sc alikuwa na kibarua kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi na kufanikisha kuondoka na pointi tatu muhimu mbele ya maafande hao.


Katika mchezo huo Simba Sc ilianza kupata mabao matatu ya kuongoza katika kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wao Kibu Dennis alifunga dakika ya 44 na Meddie Kagere ambaye amepachika mabao mawili dakika ya 17 na 36 kwenye mchezo huo.


Goli la kufutia machozi la Ruvu Shooting lilifungwa na Elias Maguli dakika ya 63.

Post a Comment

0 Comments