Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS AZINDUA HUDUMA ZA MAWASILIANO KASUMO BUHIGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Kijiji cha Kasumo wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kuzindua huduma ya mawasiliano baada ya kujengwa mnara kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). Desemba 14,2021.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizindua rasmi huduma ya mawasiliano katika Kijiji cha Kasumo wilayani Buhigwe baada ya kujengwa mnara kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). Desemba 14,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Viongozi na wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa huduma ya mawasiliano baada ya kujengwa mnara kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Kijiji cha Kasumo wilayani Bugigwe mkoa wa Kigoma. Desemba 14,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiagana na wananchi mbalimbali wakati akiondoka mara baada ya kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa huduma ya mawasiliano baada ya kujengwa mnara kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).katika Kijiji cha Kasumo wilayani Buhigwe mkoa wa Kigoma. Desemba 14,2021.

***********************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewasihi watanzania kutumia vema mawasiliano katika kujiletea maendeleo ikiwa pamoja na kupata maarifa mapya ya kilimo, ufugaji pamoja na biashara.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua huduma ya mawasiliano katika kata ya Kajana Kijiji cha Kasumo wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, huduma iliofikishwa na shirika la mawasiliano nchini TTCL kwa kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Amesema serikali inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano hasa maeneo ya mipakani ili kuharakisha maendeleo ya wananchi pamoja kuongeza ulinzi na usalama katika maeneo hayo. Makamu wa Rais amesema uwepo wa huduma za intaneti hasa katika maeneo ya vijijini ni kichocheo kikubwa cha kuboresha huduma za kijamii pamoja na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii katika taifa.

Amewasihi wananchi wa Vijijini vilivyonufaika na mawasiliano hayo kutumia katika kujitengenezea ajira ikiwemo kuanzisha biashara bunifu zinazotokana na uwepo wa mawasiliano.

Aidha Makamu wa Rais amewataka wananchi wa Kasumo kutumia mawasiliano hayo kutoa taarifa muhimu zikiwemo za wahamiaji haramu, uhalifu pamoja na ajali za kimiundombinu kama ya umeme ili kusaidia serikali kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na changamoto hizo.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewataka wananchi wa maeneo hayo kulinda miundombinu ya mawasiliano iliowekwa kwani kuhujumu miundombinu hiyo ni kujirudihsha nyuma kimaendeleo. Amesema serikali inatumia gharama kubwa katika kuwafikishia wananchi mawasiliano hasa maeneo ya vijijini hivyo jukumu la ulinzi wa miundombinu hiyo ni la kila mwananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknlojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na wote wanaotumia vibaya mawasiliano ikiwemo kufungia jumla ya laini za simu 64928 pamoja na kufungia namba za utambulisho 50703 ambazo zilizuiliwa kusajili kutokana na kutumika kusajili namba zilizoshiriki katika uhalifu.

Waziri Dkt Kijaji amesema wizara itaendelea kulisimamia shirika la mawasiliano kwa ukaribu ili liweze kujiendesha kwa faida pamoja na kuongeza wateja wa ndani na nje ya nchi , kuongeza uwajibikaji katika kutoa huduma pamoja kuongeza mapato ya shirika na serikali kwa ujumla.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Nchini Waziri Kindamba amesema TTCL imetatua changamoto kubwa iliowakabili wananchi wa Kasumo kwa muda mrefu ya kushindwa kutumia huduma za kifedha pamoja na Intaneti katika simu zao za mkononi huku Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba amesema miradi ya mawasiliano inaendelea katika kata 1068 nchi nzima ili kuhakikisha maeneo ya vijijini na yale ya pembezoni mwa nchi yanapata mawasiliano.

Post a Comment

0 Comments