






(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC ) wametakiwa kujiandaa kwenda na mabadiliko yatayojitokeza katika soko kwa mwaka mpya wa 2022 ili kuweza kuinua na kuendelea kuwa juu Shirika hilo.
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw.Elirehema Doriye wakati wa mkutano wa kufunga mwaka uliofanyika katika ukumbi wa NIC Jijini Dar es Salaam.
Amesema mwaka mpya wa 2022 watendaji wa NIC Wanatakiwa kuwa na mtazamo mpya,utendaji wenye ubunifu na uadilifu wa hali ya juu ili kuwahudumia watanzania kwa kiwango chenye ubora uliotukuka.
" Kuanzia mwaka 2002 NIC imekuwa ikikuwa katika utoaji huduma zake mpaka hivi leo lakini mwaka ujao unapaswa kuwa bora zaidi kushinda miaka yote ilyopita kwa kuongeza ufanisi katika kazi ikiwa ni pamoja na juhudi binafsi" Amesema Bw.Doriye.
Amesema jambo la kumshukuru Mungu kumaliza mwaka wakiwa salama na wamoja katika utendaji kazi ambao umekuwa chachu katika ujenzi wa taifa.
0 Comments