Ticker

6/recent/ticker-posts

SHERIA KWA MUWEKEZAJI KUWA NA UWEZO WA KULETA WAGENI 10 WATAKAOWEZA KUFANYA KAZI NCHINI NI URSA KWA WATANZANIA

Kamishna wa Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge ,Uratibu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ) Brigadia Jenerali Frances Ronald Mbindi akizungumza wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge ,Uratibu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ) Brigadia Jenerali Frances Ronald Mbindi akizungumza wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao cha kupata mrejesho kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge ,Uratibu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ) Brigadia Jenerali Frances Ronald Mbindi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu imesema Sheria kwa Muwekezaji kuwa na uwezo wa kuleta wageni Kumi watakaoweza kufanya kazi nchini ni fursa kwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu Brigadia Jenerali Fransis Ronald Mbindi wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Brigadia Jenerali Fransis Mbindi amesema lengo na mabadiliko hayo ni kuhakikisha fursa za Jira kwa Watanzania zinaongezeka ambapo kila raia mmoja wa Kigeni ataajiri raia kumi Wakitanzania.

Amesema Sheria ya kuratibu ajira za Wageni ilifanyiwa marekebisho ya Kwanza tangu ilipotungwa mwaka 2015 na Bunge la Bajeti huku akitumia kifungu namba 16 cha Ajira kuwataka waajiri kuwasilisha mawasilisho ya majina ya raia wa kigeni walionao kwa Kamishna wa kazi kabla ya Desemba 31.

Pamoja na hayo ameongeza mabadiliko mengine yamefanyiaka kupitia Bunge lililopita Octoba 2021 amabapo kuna baadhi ya vipengele katika sheria vimebadilishwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Biashara hapa nchini ikiwa ni pamoja na muda wa kibali cha Kazi .

Mfumo wa Kieletroni wa kushughulikia vibali vya maombi ya vibali vya kazi kwa wageni ulianza kutumika April 23 , 2021.

Post a Comment

0 Comments