Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA CANAF 2021 KUBAKI TANZANIA NI LAZIMA , NJOONI TUISHANGILIE TEMBO- BASHUNGWA.

Na. John Mapepele


Waziri mwenye dhamana ya nchini, Mhe. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wadau wa Michezo nchini kujitokeza kwa wingi leo Disemba 2, 2021 kuishangilia timu ya Tanzania ya soka ya wenye ulemavu (Tembo Warriors) katika mchezo wake wa nusu fainali na timu Liberia ili waweze kutwaa kombe la mashindano ya Bara la Afrika ya soka kwa wenye ulemavu CANAF 2021.


Mhe. Bashungwa ametoa wito huo leo kufuatia timu ya Tembo Warriors jana kufuzu mashindano ya dunia ya mchezo huo yatakayofanyika Oktoba 2022 nchini Uturuki.


"Tunamshukuru Mungu kazi ya kwanza ya kufuzu kwenda kombe la dunia tumeifikia jana kwa kuwa timu ya kwanza kufuzu, kazi ya leo tunahakikikisha tunaibamiza Liberia, ili tufike fainali na kulibakiza kombe nchini ili kuliheshimisha taifa letu nitoe wito kwa watu wajitokeze kuishangilia kwa wingi na kuipa hamasa timu yetu iendelee kushinda" ameeleza, Mhe. Bashungwa.


Aidha, amefafanua kwamba timu ya Tembo Warriors imeandika historia ya kuwa timu ya kwanza ya soka Tanzania kabla na baada ya Uhuru kuingia kombe la dunia.


Amesema kutokana na umuhimu wa michezo hiyo aliamua kuteua Kamati maalum ya kitaifa ili kuratibu maandalizi yote ya timu ya Tembo Warriors ili ishinde iliyosimamiwa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara yake Dkt. Hassan Abbasi


Mikakati tuliyojiwekea kama Wizara ilikuwa kufanya maandalizi ya kimkakati , pia napenda kumshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuongoza vema kwenye kipindi chote cha maandalizi haya ambapo siku mbili kabla ya mashindano kupitia Mhe. Waziri Mkuu alitoa salam na kuichangia timu milioni 150 kwa ajili ya maandalizi hayo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Michezo nchini, Yusufu Omary Singo amesema Timu nne zimefanikiwa kuingia nusu fainali kwenye Mashindano hayo.


Ametaja timu zilizoingia kwenye mzunguko wa nusu fainali na makundi yatakavyocheza leo Disemba 2, 2021 kuwa ni
(Tanzania vs Liberia) na (Angola vs Ghana ) 


Michezo hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa kumi jioni


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa wenye ulemavu Peter Sarungi amesema timu imeendelea kuwa na morali kubwa ya kushinda mechi ya kesho kutokana na ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini.


Sarungi amemuahidi Mhe. Rais Samia na wapenda Michezo wote nchini kupambana ili kutwaa kombe hilo.


Waziri Bashungwa alipokuwa akizindua mashindano ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu CANAF 2021 Novemba 2021 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments