Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AZINDUA RASMI MRADI WA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA BANDARI YA GATI NAMBA 0-7 BANDARINI JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria ufunguzi Rasmi kwa ajili ya matumizi ya mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika Bandarini Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Eric Hamissi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kufungua rasmi kwa ajili ya matumizi ya mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Eric Hamissi kuhusu Ujenzi wa gati namba 0 hadi 7 kabla ya kuzindua rasmi kwa ajili ya matumizi katika hafla iliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Eric Hamissi kuhusu uongezwaji wa kina cha bahari katika lango kuu la kuingia katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Eric Hamissi pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa kuhusu shughuli mbalimbali za Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika Bandari hiyo ya Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kufungua rasmi kwa ajili ya matumizi Mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021

Post a Comment

0 Comments