Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA NCHINI WATAKIWA KUTOPANDISHA BEI YA BIDHAA ZAO KATIKA MSIMU HUU WA SIKU KUU.***********************

Wafanyabiashara nchini, wametakiwa kutopandisha bei za bidhaa mbalimbali katika msimu huu wa sikukuu ili kuwasaidia wananchi kupata mahitaji na kufurahia sikukuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akifungua duka la nguo la LC Waikiki, Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof Kitila Mkumbo, amesema Duniani kote kipindi cha sikukuu ni kipindi cha kufanya punguzo la bei na sio kupandisha bei

Alisema wafanyabiashara wanapaswa kufuata bei elekezi ama kuuza kwa bei halali katika kipindi chote cha mwaka bila kujali kunanini ili kutowakandamiza wananchi.

"Wakati wa sikukuu wafanyabiashara duniani kote wanafanya punguzo la bei za bidhaa na sio kupandisha, ilikuwasaidia watu kupata mahitaji."

"Niwatake wafanyabiashara wa vyakula nguo na bidhaa mbalimbali kupunguza bei ilikusaidia wananchi wafurahie msimu wa sikukuu."alisema prof Kitilya

Pia amewapongeze wamiliki wa LC Waikiki kwa kutoa na kuongeza ajira kwa watanzania wapatao 50 na kuongeza uchumi wa nchi .

Lc waikiki duniani kote wanamaduka 1152 na hili walilolifungua sasa ni duka la 1153.

Post a Comment

0 Comments