Ticker

6/recent/ticker-posts

DC MULEBA AZINDUA HUDUMA YA MELI YA MATIBABU (MEDICAL SHIP) MV.JUBILEE HOPE KWA WAKAZI WA VISIWANI


MKUU wa wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Toba Nguvilla akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Meli ya Matibabu (Medical Ship) Mv.Jubilee Hope.
MKURUGENZI wa Halmahsuri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila katika akipata maelezo kuhusu namna huduma mbalimbali zinavyotolewa ndani ya meli hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye meli hiyo.

***************

NA MWANDISHI WETU,KAGERA

MKUU wa wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Toba Nguvilla amezindua huduma ya Meli ya Matibabu (Medical Ship) Mv Jubilee Hope kwa wakazi wa Visiwani hivyo ili kuweza kuondokana na changamoto ambazo walizokuwa wanakumbana nazo wananchi awali.

Uzinduzi wa meli hiyo ya matibabu ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Elias Mahwago Kayandabila na viongozi wengine ambao wamefurahia uwepo wa huduma hiyo muhimu.

Hatua hiyo inatajwa kwamba itakuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo yenye Kata 43 huku kata 5 za Mazinga, Ikuza, Bumbile, Kerebe na Goziba zikiwa ndani ya Ziwa Victoria na kwa ujumla wake inakadiriwa kuwa na wakazi takribani 68,000 kwa majibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu huyo wa wilaya alisema uwepo wa meli hiyo ni ukombozi wa matibabu kwa wananchi wa maeneo hayo kutokana na awali kutokuwa na kituo cha afya hata kimoja kwenye kata hizo jambo ambalo limepelekea halmashauri kuja na ubunifu wa meli ya matibabu kama mkakati wa muda mfupi.

Alisema meli hiyo Mv. Jubilee Hope inatarajiwa kuzunguka visiwa vyote 26 ambavyo vinakaliwa na watu ili kutoa huduma mbali mbali kwa wananchi wa Muleba waishio visiwani.

Mkuu huyo wa wilaya alisema tayari wilaya ya Muleba imeanza kutekeleza mkakati wake wa muda mrefu wa kujenga Kituo cha Afya kwa Kila Kata iliyoko Kisiwani ambapo tayari Tsh. Milioni 350 fedha za mapato ya ndani zimetolewa Kata ya Bumbile ili kujenga Kituo cha Afya.

Ambapo lengo kuu lilikuwa ni kupeleka fedha kiasi cha Milioni 500 kwa mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 huku uzinduzi wa meli hiyo ya matibabu ulifanywa na Mkuu huyo wa wilaya kwenye Kisiwa cha Chakazimbwe kilichopo Kata ya Ikuza.

Mkuu huyo wa wilaya alisema meli hiyo ya matibabu inatarajiwa kutoa huduma katika kipindi cha miaka 5 kuanzia sasa na itatumia takribani Tsh. 1.5bilion ambazo zimechangiwa na Serikali (Halmashauri ya Muleba), Taasisi ya Vine Trust ya Uingereza, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Na Kanisa la AICT ambao wamekuwa kiungo muhimu sana katika upatikanaji wa Meli.

Kwa kutambua umuhimu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imeamua kusajili Meli hiyo kama Kituo cha Afya kwa upande wa ziwani ambapo Tsh. 119 milioni zimelipwa MSD ili kupata uhakika wa madawa kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments