Ticker

6/recent/ticker-posts

MASHABIKI 10 WA KWANZA KUCHANJA KUSHUHUDIA MTANANGE WA SIMBA SC NA MTIBWA SUGAR MANUNGU


***************

Na. WA - MOROGORO

Kufuatia mtanange unaotarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi Januari 22, 2022 kati ya Simba Fc na Mtibwa Sugar Mashabiki wa timu za mpira wa miguu wameshauriwa kupata chanjo ya UVIKO-19 na watu 10 wa kwanza watapata tiketi bure.

Ushauri huo umetolewa na Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifalu katika uwanja wa Manungu, Turiani mkoa Morogoro.

"Kwa kutambua umuhimu wa chanjo mimi nitakuwa mtu wa kwanza kupata chanjo, hivyo niwaombe na wananchi kupata chanjo kwa kuwa ina umuhimu mkubwa." amesema Kifalu

Aidha Bw. Kifalu amesema baada ya kupata elimu juu ya UVIKO-19 ndipo alipofanya maamuzi ya kupata Chanjo ili kujikinga mwenyewe na kukinga watu wake wa karibu.

Hata hivyo Mtendaji Mkuu wa Timu ya Mtibwa Sugar Swabri Aboubakar amesema hii ni fursa kwa mashabiki 10 wa kwanza kupata huduma ya chanjo kupatiwa tiketi za kuingia kutazama mchezo huo.

"Kwa kutambua Juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan sisi kama viongozi tunawasihi wachezaji wetu na mashabiki wetu kupata chanjo ya UVIKO-19 ili tucheze kwa Furaha na kujiamini." amesema Swabri.

Nae mlinzi wa timu hiyo Abdi Banda amesema alishapata chanjo baada ya kujua umuhimu wake ili ailinde familia yake.

"Mimi nimechanja kwa kujua umuhimu wake na wewe kachanje ili ujikinge mwenyewe na uwakinge wa karibu yako." amesema Banda.

Post a Comment

0 Comments