Ticker

6/recent/ticker-posts

MHE.HEMED SULEIMAN AFUNGUA MAABARA BINGUNI

Makamo wa Pili wa Rais Mh.Hemed Suleiman Abdulla akikaata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la maabara ya utafiti na upimaji wa Virusi vya Uviko -19 katika Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) huko Binguni Wilaya ya Kati , kuelekea maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Afya, ustawi wa Jamii ,Wazee ,Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akizungumza katika ufunguzi wa maabara ya utafiti na upimaji wa Virusi vya UVIKO-19 pamoja na jengo la Ofisi ya watafiti taasisi ya utafiti wa Afya (ZAHRI) huko Binguni Wilaya ya kati Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais Mh.Hemed Suleiman Abdulla akifungua pazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la msingi Jengo la maabara ya utafiti na upimaji wa Virusi vya Uviko -19 katika Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) huko Binguni Wilaya ya Kati , kuelekea maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rai Mh.Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kufika katika Tasisi ya Utafiti wa Afya (ZAHRI) kufungua jengo la maabara ya utafiti na Upimaji wa Virusi vya UVIKO-19 pamoja na jengo la Ofisi ya watafiti katika Taasisi hiyo.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

**************************

Na Khadija Khamis –Maelezo. Zanzibar

02/01/2022

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema shabaha kubwa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia huduma Bora wananchi wake pamoja na kuhakikisha huduma za Afya zinaboreshwa.

Akiyasema hayo huko Binguni Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ufunguzi wa Jengo la Maabara ya Utafiti na Upimaji wa Virusi vya uviko 19 pamoja na maradhi mbali mbali ya mripuko ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na mafanikio ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Alisema katika kuimarisha huduma za afya ikiwemo kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Afya pamoja na kuwatatulia changamoto zao .

Amewataka watumishi hao kuzitumia mashine hizo kwa umakini na uangalifu mkubwa kutokana na gharama kubwa ya vifaa hivyo

Aidha aliwafahamisha wanasayansi chipukizi kuitumia taasisi ya utafiti ili kukuza vipaji vyao kwa manufaa yao na Taifa kiujumla

Makamu huyo akitoa shukrani kwa Taasisi za utafiti za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ikiwemo Taasisi ya utafiti na Magonjwa ya Binaadamu (National Institute of Medical Research -NIMR,) na Taasisi ya Afya ya Ifakara ,(Ifakara Health Institute -IHI ) .kwa mashirikiano makubwa waliyoyaonyesha pamoja na washiriki wa Maendelea kutoka Swiss Development Corporation na Shirika la Afya Ulimwengu Afisi ya Tanzania.

Nae Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Nassor Ahmed Mazrui amesema licha ya mafanikio mazuri yaliyopatikana lakini pia kunachangamoto mbali mbali ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi ikiwemo uhaba wa Fedha za kukamilishia majengo ya maabara ya biology na chemistry pamoja na rasilimali fedha za kuchunguzia tafiti muhimu.

Kwa upande Afisa Muendeshaji Mkuu wa Taasisi ya Ifakara Bw.Martin Mfikiwa ameridhishwa na mashirikiano na Wizara ya Afya kuhakikisha lengo lilikusudiwa linafanikiwa kwa ufanisi mkubwa.

Alieleza kuwa baadhi ya watumishi 17 wameshabatiwa mafunzo kwa vitendo ya matumizi ya mashine za kuchunguzia maradhi mbali mbali ikiwemo uviko 19.

Post a Comment

0 Comments