Ticker

6/recent/ticker-posts

MKUTANO WA 19 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA AFRIKA NA NORDIC KUFANYIKA JUNI 2022 FINLAND

Na Mwandishi Wetu, Dar

Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na nchi za Nordic unatarajiwa kufanyika mwezi Juni 2022 nchini Finland.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika kuendeleza na kuimarisho ushirikiano wa nchi hizo mbili viongozi hao wamependekeza kufanikisha ziara ya Mhe. Waziri Mulamula nchini Finland pamoja na ushiriki wake katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Nordic utakaofanyika nchini Finland mwezi Juni 2022.

Katika mazungumzo ya viongozi hao, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi Swan kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Finland katika kuhakikisha Mataifa hayo yanashirikiana kijamiii, kisiasa na kiuchumi.

"Finland amekuwa mdau Mkubwa wa Maendeleo hapa nchini kwetu hasa katika sekta ya fedha hususan katika masuala ya kodi, mazingira, tehama, uongozi pamoja na uwezeshaji wa wanawake........pia tumekubaliana kuendeleza ushirikiano wetu kwa Maendeleo endelevu," amesema Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan, wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme, Bi. Kisa Mwaseba Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments