Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI HAMZA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA OFISI ZA NEMC


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza akiongozana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe.Edward Nyamanga wakipokelewa na Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kuwasili katika Ofisi za NEMC leo tarehe 28/01/2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakijatambulisha mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza mara baada ya kuwasili katika Ofisi za NEMC leo tarehe 28/01/2022 Jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia kikao cha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza mara baada ya kuwasili katika Ofisi za NEMC leo tarehe 28/01/2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa NEMC Dkt.Samuel Gwamaka akizungumza mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza mara baada ya kuwasili katika Ofisi za NEMC leo tarehe 28/01/2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza akikabidhiwa maua kwa kukaribishwa kwenye ofisi za NEMC mara baada ya kuwasili katika Ofisi hizo tarehe 28/01/2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe.Edward Nyamanga akikabidhiwa maua kwa kukaribishwa kwenye ofisi za NEMC mara baada ya kuwasili katika Ofisi hizo tarehe 28/01/2022 Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa NEMC Dkt.Samuel Gwamaka mara baada ya kuwasili katika Ofisi za NEMC leo tarehe 28/01/2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza ametembelea ofisi ya Baraza la Uhifadhi ns Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kuahidi kuendelea kushirikiana nao ili kiweza kutatua changamoto za kimazingira zinazowakaribili wananchi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Mhe.Hamza amesema ameweza kufika NEMC kuona ni namna gani wanaweza kushirikiana katika jambo la Usimamizi na ufanyaji wa tathimini ya kuona athari athari zinazoweza kusababishwa na shughuli za kibinadamu na shughuli zingine kwenye mazingira.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema jitihada za kuendelea kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi inahitajika ili Kudhibiti uharibu wa mazingira.

"Taaluma inahitajika kwa wananchi zikiwemo shughuli za uchimbaji wa madini, shughuli za kwenye masoko na hata katika shughuli za kwenye misitu kwasababu huko kunachofanyika watu bado hawana taaluma hii ya utunzaji wa mazingira bado kuna harakati za uharibifu wa mazingira zinaendelea". Amesema Naibu Waziri Hamza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NEMC Dkt.Samuel Gwamaka ameahidi ushirikiano kwa viongozi wapya katika kuhakikisha changamoto ya kimazingira zinatatuliwa kwa wakati kwa ajili ya Ustawi wa nchi.

Post a Comment

0 Comments