Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS ALHAJ DKT.HUSSEIN MWINYI AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MAKAMU WA RAIS MSTAAF ALHAJ DKT.MOHAMMED GHARIB BILAL.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Safia Abeid Mama Mzazi wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj.Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto kwa Rais) iliofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Mjini Unguja, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ( kulia kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman, Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj.Dkt.Amani Karume na Makamu wa Pili Mstaaf Alhaj Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika maziko ya Marehemu Safia Abeid Mama Mzazi wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Dkt. Mohammed Bilal,Mtoto wa Marehemu Bw. Abeid, Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf Alhaj Balozi Seif Ali Iddi,yaliyofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid.(Picha na Ikulu) MAKAMU wa Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj.Dkt.Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi la Mama Yake Mzazi Marehemu Bi.Safia Abeid,baada ya kuweka mwili wa marehemu maziko yaliyofanyika Kijiji kwao Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo 4-1-2022.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Dkt.Mohammed Gharib Bilal, kwa kufiwa na Mama yake mzazi marehemu Safia Abeid, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Koboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Bi.Safia Abeid, Mama mzazi wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Dkt.Mohammed Gharib Bilal, maziko yaliofanyika Kijiji kwao Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments