Ticker

6/recent/ticker-posts

SHEIKH SHARIFU MAJINI AWATABIRIA NEEMA WANAWAKE KATIKA NYANJA YA KISIASA


****************

Mwaka huu wa 2022 umetajwa kuwa mwaka wa neema katika kilimo,biashara Pia umetajwa kuwa ni mwaka wa wanawake kung'ara zaidi katika sekta mbalimbali ikiwemo siasa mpaka mwaka 2031.

Hayo yamebainishwa leo Jijini na dar es salaam na sheikh sharif majini wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kupitia maono ameonakuwa Mwaka huu ni mwaka wakufanyakazi zaidi kwakuwa ni mwaka ambao kinyota ugawanyiki.


"Mwaka 2022 ulianza Siku ya jumamosi ambayo ni nyota ya mbuzi ambayo jiwe lake la bahati ni Ganet, namba zake za bahati ni 7 na 3 ambazo kimsingi hazigawanyiki hivyo mwaka huu mwaka huu mambo yake hayatoeleweka, simu ya bahati Katika mwaka huu 2022 inaangukia siku ya jumamosi" Alisema Sharif.

Aidha amesema Tanzania imepata bahati ya kuwa na rais mwanamke ambaye ni mama samia suluhu kupitia yeye taifa litapata fursa mbalimbali kimataifa kwakuwa nyota ya Samia ni yenye nguvu, mvuto, wapenda mageuzi ya kimaendeleo pia ni nyota isiyosimama na yeyeto atayejaribu kumgusa atadhurika mwenyewe hivyo kwasasa Tanzania ipo kwenye mikono salama ya mama samia.

"2022 mpaka mwaka 2031 ni kipindi cha wanawake kungara katika nyanja mbalimbali ikiwemo nyanja ya kisiasa, pia Katika kipindi cha mwaka 2022 kutakuwa na ongezeko la wanafki katika sekta mbalimbali"

Sanjari na hayo sheikh sharifu amesema Maradhi ya uviko-19 ni fimbo ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, inatukumbusha kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kumkumbuka Mungu Katika kipindi chote cha maisha.

"Maradhi haya ya Corona Bado yataendelea kuutesa ulimwengu na dawa yake itapatikana kama ilivyokuwa kwa Maradhi ya mburahati na ukoma yaliyoipiga Dunia kipindi cha nyuma ambapo dawa hiyo itatibu kwa Siku Moja Mpaka tatu.

Post a Comment

0 Comments