Ticker

6/recent/ticker-posts

UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI LITASAIDIA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022-WAZIRI NAPE

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mikoa na Halmashauri wa Tanzania Bara na Zanzibar kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na Postikodi kwa njia ya mtandao, katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo tarehe 17 Januari, 2022, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mikoa na Halmashauri wa Tanzania Bara na Zanzibar kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na Postikodi kwa njia ya mtandao, katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mikoa na Halmashauri wa Tanzania Bara na Zanzibar kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na Postikodi kwa njia ya mtandao, katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw.Waziri Kindamba akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mikoa na Halmashauri wa Tanzania Bara na Zanzibar kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na Postikodi kwa njia ya mtandao, katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw.Macrice Mbodo akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mikoa na Halmashauri wa Tanzania Bara na Zanzibar kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na Postikodi kwa njia ya mtandao, katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.

Semina ikiendelea.

(CHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye amefungua semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara na Zanzibar kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na Postikodi kwa njia ya mtandao.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Mhe.Nape amesema utekelezaji wa mfumo huo ni moja kati ya mikakati ya kuiweka nchi katika mfumo wa kidigitali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kurahisisha biashara ya mtandao.

“Mradi huu ni moja ya miradi ambapo Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuacha alama na utekelezaji wake ulitakiwa ufanyike kwa miaka mitano lakini kwa sababu ya umuhimu wake mpaka mwezi Mei mwaka huu zoezi hili litakuwa limekamilika”, Alisema Waziri Nape.

Amesema utekelezaji wa Anwani za makazi itakuwa ni zoezi ambalo litarahisisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ambayo itafanyika Agosti mwaka huu na itakuwa rahisi kwa sababu ya upatikanaji wa anwani za makazi.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa mfumo wa anwani ya makazi ni muhimu sana kwa wananchi hivyo tunalo jukumu na wajibu mkubwa ili zoezi na mfumo huu liweze kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo alieleza jinsi mfumo huu wa anwani za makazi utakavyorahisisha biashara mtandao ambapo kwa sasa Shirika la Posta lina Jumla ya maduka 600 kupitia duka lake Mtandao (Posta Online Shop) ambayo kwa uhakika yanategemea upatikanaji wa anwani za makazi katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.

 “Tumejipanga kimkakati kuhakikisha tuko tayari kwa matumizi ya anwani hizi, kwani tumeanzisha huduma ya duka mtandao ambalo limeunganishwa nchi zote duniani ambapo wananchi watakuwa wananunua na kuuza bidhaa zao duniani kote”, Macrice Mbodo.

Post a Comment

0 Comments