Ticker

6/recent/ticker-posts

UTEUZI:CCM YAMPITISHA DK.TULIA ACKSON KUGOMBEA NAFASI YA SPIKA


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Shaka Hamdu Shaka,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichofanyika leo Januari 20,2022 jijini Dodoma.

.................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

KAMATI Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM),imepitisha jina la Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Januari 20,2022 na KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Shaka Hamdu Shaka,wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shaka amesema kuwa kikao hicho kimekaa kwa taratibu na mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi ambacho kimejadili mambo mbalimbali ikiwemo majina ya waliowania nafasi ya Spika na kufikia maamuzi ya kumteua Naibu Spika wa Bunge kuwania nafasi hiyo.

"Pamoja na mambo mengine kamati hii ilipitia na kuchambua majina ya walichukua fomu za kuwania nafasi ya uspika na kumteua Naibu spika Tulia Akson kuwania nafasi hiyo ambapo kikao cha wabunge wa chama cha mapinduzi (kokasi),kitakaa Januari 30 mwaka huu na kumpigia kura,"amesema.

Aidha kamati hiyo imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, katika utendaji wake wa kazi kwa kuhakikisha wanafunzi wote nchini wameingia kidato cha kwanza kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa madarasa huku kikimpongeza Rais wa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi kutokana na utendaji wake kwa kusimamia uchumi wa bluu.

"Chama kimeridhishwa na mabadiliko Uchumi wa bluu chama kimelidhishwa na mabadiliko hayo kwahyo ccm imerdhishwaa kabis na utendaji wa serikali zote mbili

"Chama kimefuatilia kwa ukaribu sana serikali ufanyaji kazi wa Serikali na kimejiridhisha na kazi nzuri zinazofanywa na marais wapande zote mbili Bara na Zanzibar.

Mchakato wa uchukuaji fomu za kuwania nafasi ya spika ulinza Januari 10 mwaka huu na kumalizika Januari 15 mwaka huu huku walichukuwa fomu kufikia 71 na walirudisha 70 hiyo ni kufuatia aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo mnamo Januari 6 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments