Ticker

6/recent/ticker-posts

UTEUZI: RAIS SAMIA AMTEUA BI.SUZAN WILLIAM MKANGWA KUWA KAMISHNA WA KAZI


***************************


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bi. Suzan William Mkangwa kuwa Kamishna wa Kazi.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Suzan alikuwa Mtumishi katika Ofisi ya Rais Ikulu na anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Francis Ronald Mbindi aliyepangiwa majukumu mengine.

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Januari, 2022.

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Post a Comment

0 Comments