Ticker

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA VIZURI TAARIFA ZITOLEWAZO NA TMA

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete akielekezwa jambo na wataalamu wa Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo kwaajili ya kufahamiana na viongozi wa mamlaka hiyo baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibuni katika Wizara hiyo. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete akiwa katika studio za TMA mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo kwaajili ya kufahamiana na viongozi wa mamlaka hiyo baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibuni katika Wizara hiyo. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete akizungumza na watumishi wa TMA mara baada ya ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo kwaajili ya kufahamiana na viongozi wa mamlaka hiyo baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibuni katika Wizara hiyo. Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi akizungumza mara baada ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete katika Ofisi za Makao makuu ya TMA leo Jijini Dar es Salaam 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO) 

************************** 

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete amefanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania kwaajili ya kufahamiana na viongozi wa mamlaka hiyo baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibuni katika Wizara hiyo.

 Akizungumza mara baada ya kutembelea ofisi za TMA Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri huyo amesema atahakikisha anakuwa karibu na Mamlaka hiyo na kutoa ushirikiano wa kutosha ili jamii ifahamu umuhimu wa kuwepo Mamlaka hiyo ambayo inatambulika kkatika ukanda wa Afrika Mashariki kwa ubora wake. 

Amesema Watanzania wanatakiwa kutumia vizuri taarifa zinazotolewa na TMA kwa kuwa taarifa hizo ni za uhakika na kuacha kufuata porojo zinazozagaa mitaani kuwa Mamlaka hiyo haifanyi kazi kwa ufasaha.

 "Serikali inatambua umuhimu wa TMA nchini, hivyo Mhe. Rais. Samia Suluhu Hassan kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha, ametenga jumla ya Tsh. Bil. 30 ili kukamilisha mtandao wa rada saba nchini". Amesema Mhe.Mwakibete.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi amesema Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ni taasisi ya Muungano iliyoanzishwa kwa sheria Na. 2 ya mwaka 2019 ikifanya kazi zake Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar chini ya usimamizi wa Bodi ya TMA (Governing Board). 

Nae Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi amesema TMA imeendelea kujenga uwezo wa wataalamu kwa lengo la kuongeza uwezo katika nyanja mbalimbali za hali ya hewa wanazofanyia kazi ili kutoa huduma bora kwa wadau na watumiaji wa huduma za hali yya hewa.

Post a Comment

0 Comments