Ticker

6/recent/ticker-posts

BASHUNGWA AMPONGEZA MKURUGENZI WA DART DKT.EDWIN MHEDE KWA KUONGEZA MAPATO

WAZIRI wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akizungumza na na Menejimenti ya taasisi ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) alipofanya ziara katika Ofisi za Wakala hiyo pamoja na kutembelea miundombinu inayotoa huduma na ile inayoendelea kujengwa, ili kuona mapato na maendeleo ya mradi kushoto anayemsikiliza ni Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede.
Picha mbalimbali zikionesha Wazriri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa, Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe wakipata maelezo kutoka kwa Mohamed Kuganda Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji DART wakati alipokagua miundombinu ya shirika hilo.
Wazriri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa kulia na Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede kwa pamoja wakati waziri huyo akifanya ziara ya kukagua miundombinu ya DART.
Baadhi ya mabasi ya DART yakiwa yameegeshwa katika karakana hiyo hiyo mpya ya DART iliyopo Ubungo
Wazriri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa, Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe wakitoka mara baada ya kukagua karakana hiyo ya DART ubungo.
Wazriri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akigawa tiketi alizozinunua kwa kwa baadhi ya maofisa wa DART wakati alipotumia usafiri wa DART akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu kulia ni Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede
Wazriri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa na Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede wakikaguliwa kabla ya kuingia kwenye basi.
Wazriri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa na Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa vitengo wakiwa katika usafiri wa basi la DART kutoka Ubungo kwenda Gerezani.
Baadhi ya abiria wakipanda mabasi ya DART Gerezani.
Wazriri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa, Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe wakifanya ukaguzi kituo kikuu cha DART Gerezani.
.............................................

WAZIRI wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amempongeza Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk Edwin Mhede kwa kuendelea kuboresha njia za ukusanyaji mapato sambamba na kuwafichua wale wote wanaohusika na upotevu wa mapato hayo. kwa kuiwezesha taasisi hiyo kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato yake kwa zaidi ya asilimia 120.

Amesema kutokana na usimamizi mzuri DART ina kila sababu ya kuhakikisha mapato inayokusanya yanaongezeka na kuvuka wastani huo.


Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati akizungumza na Menejimenti ya taasisi hiyo alipofanya ziara katika Ofisi za Wakala hiyo pamoja na kutembelea miundombinu inayotoa huduma na ile inayoendelea kujengwa, nia ni kuona mapato hayo yanasaidia maendeleo ya mradi huo sanjari na taifa kwa ujumla.


"Niwapongeze kwa hatua hiyo lakini sasa muone haja ya kuvuka zaidi ya malengo hayo ikibidi muweke malengo ya juu zaidi ya yale mliyojiwekea awali jambo ambalo naamini mnaweza kulitekeleza" amesema Waziri Bashungwa

Amesema nia ya Serikali ni kuona miradi hiyo inazidi kuleta tija nchini na baadae iweze kuunganisha upatikanaji wa huduma za usafiri katika maeneo mengi ya ndani na nje ya Dar es Salaam suala litakaloleta ufanisi katika utoaji wa huduma.


Aidha amemtaka Mkurugenzi wa DART kuhakikisha wanaendelea kubuni mbinu mbalimbali za utoaji wa huduma sambamba na kuona namna ambavyo watashirikiana na sekta binafsi katika utoaji wa huduma ili kuongeza ufanisi zaidi.


Awali akitoa taarifa ya utendaji wa shirika hilo kwa Waziri Mkurugenzi wa DART Dk. Edwin Mhede amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 wakala umepanga kitumia kiasi cha Sh Bilioni 7.02 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vyake ambapo kati ya fedha hizo Sh Bilioni 6.72 ni matumizi ya kawaida na Sh Bilioni 298 ni kwa ajili ya ukarabati wa kawaida wa miundombinu ya awamu ya kwanza.

Amesema katika fedha hizo kiasi cha Sh. Bilioni 7.02, Sh Bilioni 2.25 ni ruzuku kutoka Serikali Kuu na Sh. Bilioni 4.76 ni mapato ya ndani huku katika kipindi cha Julai hadi Desemba wakala huyo akikusanya kiasi cha Sh. Bilioni 4.5 sawa na asilimia 128.43 ya malengo ya kukusanya Sh Bilioni 3.5.

Ameongeza kuwa kwa sasa wanaendele na ukamilishaji wa miundombinu kutoka Gerezani hadi Mbagala ambayo hadi Desemba mwaka jana ujenzi wake ulifikia asilimia 44.4 na matarajio ifikapo Machi Mwakani mradi uzinduliwe na uanze kutoa huduma.

Katika hatua nyingine pia Mtendaji huyo wa DART amesema kwa sasa wapo katika mkakati wa muda mfupi wa kuongeza mabasi 95 na hivyo kufikisha idadi ya mabasi 305 yanayohitajika katika awamu ya kwanza ya utoaji wa huduma hizo za usafiri.

Post a Comment

0 Comments