Ticker

6/recent/ticker-posts

BARRICK YATANGAZWA KINARA WA KULIPA KODI KATIKA SEKTA YA MADINI NCHINI


Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi tuzo ya Mlipa kodi mkubwa katika sekta ya madini, Meneja wa Barrick nchini Georgia Mutagahywa wakati wa hafla ya usiku wa mlipa kodi, kushoto ni Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko.

***
Kampuni ya madini ya Barrick Gold Corporation,imetangazwa kuwa kampuni inayoongoza kuchangia pato la Taifa katika sekta ya madini nchini katika kipindi cha mwaka 2021 na imetunukiwa tuzo ya mlipa kodi bora.

Tuzo hiyo ilitangazwa na kutolewa wakati wa hafla ya Usiku wa Madini ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne nchini, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali na wadau kutoka katika sekta ya madini.

Barrick ni mchangiaji mkubwa katika wa pato la Serikali kupitia ulipaji wa kodi mbalimbali na mdau mkubwa wa kuchagia uchumi wa kijamii kupitia mtandao wa biashara zake, pia imekuwa mstari wa mbele kufanikisha miradi ya kusaidia jamii katika maeneo yanayozunguka migodi yake ya Bulyanhulu,Buzwagi na North Mara.

Akizungumza na vyombo vya habari vya hapa nchini karibuni, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow alisema kampuni imetumia zaidi ya dola bilioni 1.8 katika kodi, mishahara na malipo kwa wafanyabiashara wa ndani. Pia imewekeza dola milioni 6.7 katika miradi ya elimu katika jamii, afya na miundombinu.

Migodi pia iliendelea kuajiri na kuwapatia ujuzi Watanzania. Asilimia 97% ya wafanyakazi ni watanzania , huku 41% wakitoka katika vijiji vinavyoizunguka. Pia imeimarisha ushirikiano na wazabuni wa ndani.

Mbali na Tuzo ya Mlipa kodi bora,kampuni imetunukiwa tuzo mbalimbali.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi moja ya tuzo hizo Meneja Uhusiano wa Barrick  Neema Ndossi kwa niaba ya kampuni katika hafla hiyo.  kushoto ni Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko.
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo mbalimbali ambazo kampuni imejishindia.

Post a Comment

0 Comments