*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imefanya kufuru kwa kufanikiwa kuinyuka timu ya Ruvu Shooting kwa mabao 7-0 kwenye kombe la Azam Sport Federation Cup (ASFC) mechi iliyopigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jjijini Dar es Salaam.
Clatous Chama au muite Tripple C ambaye alikuwa mwiba kwenye mechi hiyo mara baada ya kupiga mabao matatu (Hat Trick) na kuiwezesha timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 7-0.
Dakika ya kwanza tu ya mchezo iliwafanya Simba Sc kupata bao la mapema la kuongoza kupitia kwa kwa mshambuliaji wao John Bocco ambaye pia kwenye mchezo huo aliweza kupachika mabao mawili ambapo bao lingine alilifunga dakika ya 39 ya mcezo.
Mpaka kippindi cha kwanza kinamalizka Simba Sc alikuwa mbele kwa mabao 5-0 ambapo mlima ulikuwa mkubwa kwa Ruvu Shooting kufanya uwezekano wa kurudisha mabao hayo.
Mabao mengene yaliwekwa kimyani na Jimmyson Mwanuke dakika ya 70, Clatous Chama dakika ya 25,27,72 na bapo lingine Ruvu Shooting wakijifuunga kupitia kwa Michael Masinda.
0 Comments