Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMPYUTA 300 ZIMETOLEWA KWA VYUO 35 VYA UALIMU ILI KUBORESHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHIA NCHINI.WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga ,akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Caroline Nombo,akitoa taarifa ya wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.


Wakuu wa vyuo mbalimbali wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akiangalia Kompyuta kabla ya kuzikabidhi kwa wakuu wa vyuo wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akiwakabidhi Kompyuta baadhi ya wakuu wa vyuo wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.


Mkuu wa Chuo cha Marangu TC Dk.Colonel Chambulila,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) mara baada ya kukabidhi Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa hafla iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.

............................................................

Na Zena Mohammed,Dodoma.

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema ili kuhakikisha uandaaji wa walimu unakuwa wa kisasa Wizara yake kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu nchini (Teacher Education Support Project (TESP) imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Ualimu iliviweze kukidhi maendeleo yaliyopo ya Sayansi na Teknolojia.

Prof.Mkenda amesema hayo jijini hapa leo wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa huku vyuo 13 vikipata Kompyuta 50 ambapo ,Vyuo 4 vimepata Kompyuta 30 na Vyuo 09 Kompyuta 20 na Vyuo vyote 35 vitapatiwa Kompyuta Mpakato moja kwa ajili ya kusaidia idara zingine vyuoni.

"Leo mtapatiwa Kompyuta za Mezani na Kompyuta Mpakato na Mgao wa kompyuta hizi umezingatia uwiano kati wanachuo na vifaa vilivyopo katika Vyuo vyetu kwa sasa,"amesema.

Amesema dhima ya Vyuo vya Ualimu nchini ni kuandaa walimu mahiri na wanaotosheleza mahitaji katika shule za Awali, Msingi na Sekondari.

"Kutokana na dhima hiyo, Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika Vyuo vyote vya Ualimu vya Serikali nchini mkazo ukitolewa katika uboreshaji wa miundombinu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na matumizi ya TEHAMA kama nyenzo muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji. Uboreshaji huu unakwenda sanjari na maendeleo makubwa katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika ufundishaji na Ujifunzaji,"Amesema. Hata hivyo amesema Wizara inaendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika Vyuo mbalimbali nchini ikiwemo ukamilishaji wa Chuo cha Kabanga, Ujenzi wa vyuo vipya vya Sumbawanga, Dakawa, Mhonda na Ngorongoro unaendelea.

Aidha amesema kuwa ukarabati na ujenzi wa baadhi ya miundombinu katika vyuo vya Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Kasulu, Butimba na Patandi nao unaendeleana huku ukitarajiwa kukamilika mwaka huu wa fedha 2021/2022.

"Hadi sasa Wizara imetoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA katika kufundishia na kujifunzia kwa wakufunzi wote 2,300 kutoka Vyuo vya Ualimu vya Serikali yote 35 na mtakumbuka kuwa, Wizara imekwisha gawa vifaa vya TEHAMA ikiwa ni Kompyuta za Mezani (Desktop) 1,120, Kompyuta za mkononi au Kompyuta Mpakato (laptop) 113, na Projekta 186 ambapo Vifaa hivi viligawiwa kwa Vyuo vyote 35 vya Ualimu, hivyo vifaa vya leo ni nyongeza ili kukidhi mahitaji,

"Hii itasaidia kupunguza uwiano wa matumizi ya kompyuta kwa Wanachuo kutoka Wanachuo 28 kwa Kompyuta moja hadi kufikia Wanachuo 2 kwa Kompyuta 1 vyuoni,"amesema.

Pamoja na hayo amewaagiza wakuu wa vyuo hao kutunza Kompyuta hizo ambapo amesema Kompyuta hizo zimenunuliwa kwa gharama kubwa hivyo kila Mkuu wa Chuo kuhakikisha kuwa zinatumika kwa malengo ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji Chuoni.

"Kila Mkuu wa Chuo ahakikishe mali zote za Serikali zinatunzwa ipasavyo ili kuleta tija ya fedha zilizotumika na Vyuo vyote vya Ualimu vizingatie matumizi sahihi ya kompyuta hizi ikiwemo kuhaikikisha ziko katika mazingira yaliyo safi na salama kama ilivyo kanuni na taratibu za kutunza na kuhifadhi vitu vya TEHAMA,"amesema.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia,Prof.Carolyne Nombo amesema mchango wa serikali ya Canada katika mradi huu ni jumla ya Dola za Canada milioni 53 kama mchango kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshaji wa vyuo zikiwemo gharama za malipo ya chakula kwa wanachuo na gharama za mafunzo ualimu kwa vitendo.

Amesema matumizi ya fedha hizo ni pamoja na Kuwajengea uwezo Menejimenti za vyuo vya Ualimu vya Serikali juu ya Usimamizi wa Vyuo husika, Kuwezesha uandaaji wa Kanzi Data (Data base) ya Elimu ya Ualimu (Pre service teacher education management information system),Kuwezesha maandalizi ya Kiunzi cha Umahiri kwa Wakufunzi na Walimu nchini na Kugharimia kazi mbali mbali za Kitaalamu ikiwemo utoaji wa Elimu ya Usawa wa Kijinsia katika Elimu ya Ualimu.

Pia Ujenzi mpya Chuo cha Ualimu Kabanga kilichopo katika,Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma,Kujenga Kituo Kikubwa cha kuendeleza somo la Hisabati katika Chuo cha Ualimu Dakawa na kukarabati jengo,litakalotumika kama kituo cha muda cha Kuendeleza somo la Hisabati katika chuo cha Ualimu Morogoro na Kujenga, Kukarabati na Kuweka Samani katika Maabara za Sayansi, TEHAMA na Maktaba katika vyuo vya Ualimu.

Na Vyuo saba vya awali vilinavyoendelea ukarabati na ujenzi ni Chuo cha Ualimu Butimba, Morogoro, Mpwapwa,Tukuyu, Kasulu, Patandi na Dakawa.

Post a Comment

0 Comments