Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA SULUHU ATUMBUA WAKURUGENZI WANNE WA HALMASHAURI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza alipokua njiani akielekea Mkoani Mara leo Tarehe 04 Februari 2022.

************************

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Februari 4, 2022 akiwa njiani Magu jijini Mwanza akielekea Musoma mkoani Mara ametengua uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo na upotevu wa mapato katika halmashauri hizo.


“Siku ile tunazitangaza fedha nilisema kama mkurugenzi anataka kuona rangi yangu halisi achezee hizo fedha, sasa kwa traarifa zilizopo, Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini, wakurugenzi wamechezea fedha. Mheshimiwa waziri (Waziri wa Tamisemi) wakurugenzi hao nimewatengua sasa hivi” amesema Rais Samia na kuongeza

“Yule wa Geita endeleeni na uchunguzi, na mimi timu yangu iko pale inafanya uchunguzi naye wakiniletea na makossa kama haya nay eye attatenguliwa” amesema


Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa alisema kuwa Wizara hiyo ilipata taarifa za ubadhirifu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu Wilaya ya Buchosa na maeneo mengine.


Waziri Bashingwa alianza kwa kutoa pongezi kwa Rais Samia kutokana na ujenzi wa madarasa ya fedha za Uviko-19.

Baada ya kumaliza, Rais Samia alimuagiza Waziri Bashungwa kutaja maeneo mengine ambayo kumefanyika ubadhirifu.


“Hivi sasa Ofisi ya Rais Tamisemi tunafanya uchunguzi katika halmashauri ya Jiji la Mbeya, Singida, Iringa Mjini” amesema Bashungwa

Post a Comment

0 Comments