Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA AFYA YATOA MAFUNZO YA CHANJO KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA NA SIMIYU

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye kikao cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waandishi wa habari wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha masuala ya chanjo ikiwemo chanjo dhidi ya UVIKO -19.

Rai hiyo imetolewa leo Ijumaa Februari 4,2022 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga na Simiyu kwa ajili ya uhamasishaji kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo chanjo ya Chanjo ya UVIKO – 19 ili kulinda afya za wananchi.

Dkt. Ndungile amesema kuwa waandishi wanayo nafasi kubwa ya kutoa habari na kuwahamasisha wananchii kuhusiana na chanjo kwani wananchi wana imani na vyombo vya habari.

"Msiishie kuandika stori ya leo tu bali mkawe mabalozi wa kuandika habari za chanjo kila mara. Naomba mkawe mstari wa mbele kuhamasisha masuala ya chanjo na wale ambao hawajachanja wachanje ili wawe chachu ya mabadiliko kwani wana wajibu wa kufikisha taarifa sahihi kwa jamii",amesema Dkt. Ndungile.

“Leo tumekutana hapa kujadili kuhusu chanjo na wajibu wa mwandishi wa habari kuhamasisha masuala ya chanjo. Kikao cha leo kikazae matukio mbalimbali ya chanjo. Tumeona kuna chanjo zaidi ya 10 hivyo unaweza ukawa unazungumzia chanjo moja kila mwezi mfano chanjo ya kuzuia chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi”,amesema Dkt. Ndungile.

 Amezitaja miongoni mwa chanjo zinazotolewa nchini Tanzania ni pamoja na chanjo ya UVIKO - 19, Kifua Kikuu (BCG),Polio (OPV), Polio (IPV), Surua Rubela (MR), (Donda koo,kifaduro,pepo punda, homa ya ini homa ya uti wa mgongo, homa ya mapafu -Pentavalent), Pepo punda kwa wajawazito, saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV), Nimonia (PCV13) na Kuhara Kukali ( Rota).

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wameiomba serikali kushirikiana kwa ukaribu na waandishi wa habari kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara bila kuyasahau makundi mengine katika jamii wakiwemo viongozi wa dini, siasa,mila na wasanii wa nyimbo za asili kwani wana ushawishi mkubwa katika jamii.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19 kilichofanyika leo Ijumaa Februari 4,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Afya, Catherine Sungura akizungumza kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19
Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo - Wizara ya Afya, Lotalis Gadau akitoa mada kuhusu chanjo mbalimbali kwenye mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga  kuhusu masuala ya chanjo.

Kikao kinaendelea

Mratibu wa Chanjo ya UVIKO- 19 Mkoa wa Shinyanga, Timothy Sosoma akiwa ukumbini
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments