..............................................
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao: -
Amemteua Mhandisi John Gervas Nzulule kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).
Bwana Zulule ni Mhandisi Mwandamizi, TGFA.
Amemteua Dkt. Selemani Budeba Majige kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya PUMA Energy Tanzania Ltd.
Bwana MAJIGE anaendelea kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (03).
Amewateua Bw. Peter llomo na Bibi Suzan Mlawi kuwa Wajumbe wa Baraza la Maadili katika Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka mitatu (03).
Uteuzi huu umeanza tarehe 03 Februari, 2022.
0 Comments