Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Nane ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) pamoja na kuikabidhi vitendea kazi ili kutekeleza majukumu yao ya kiutendaji uliofanyika leo Februari 4,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nane ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC), Prof. Esnati Chaggu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo leo Februari 4,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimkabidhi kitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Nane ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC), Prof. Esnati Chaggu mara baada ya kuizindua bodi hiyo leo Februari 4,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Nane ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) pamoja na kuikabidhi vitendea kazi ili kutekeleza majukumu yao ya kiutendaji uliofanyika leo Februari 4,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Bodi ya Nane ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) pamoja na kuikabidhi vitendea kazi ili kutekeleza majukumu yao ya kiutendaji uliofanyika leo Februari 4,2022 jijini Dodoma.
................................................................
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo ameiagiza Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) , kupitia muundo na majukumu ya Baraza hilo ili kuangalia utekelezaji wake.
Aidha ameagiza kuhakikisha mfumo wa vibali vya taka hatarishi unatengenezwa ndani ya siku 45.
Maagizo hayo ameyatoa leo Februari 4,2022 jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Nane ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na kuikabidhi vitendea kazi ili kutekeleza majukumu yao ya kiutendaji.
Dkt.Jafo amesema kuwa bodi ya NEMC ni chombo muhimu kinachoishauri Serikali katika masuala muhimu ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
''Namtaka Mwenyekiti wa Bodi hii kuhakikisha anasimamia suala la mfumo na ndani ya siku 45 mchakato wa mfumo huo uwe umekamilika.''amesema Dk.Jafo
Waziri Jafo ameitaka Bodi hiyo, kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mazingira ya Mwaka 2021, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Serikali.
Ameaagiza kupitia upya muundo na majukumu ya Baraza ili kuimarisha utendaji wake na kutatua changamoto zilizopo katika suala zima la uhifadhi na usimamizi wa mazingira na kutoa ushauri ipasavyo.
“Kama mnavyofahamu Sera Mpya ya Mazingira ya mwaka 2021 inategemea kuzinduliwa Februari 12, mwaka 2022 na sera hii inatoa miongozo ya kisera katika kutatua changamoto mpya za mazingira zinazoikabili nchi yetu,”amesema
Aidha amewataka kusimamia mapato na matumizi ya fedha na kulisimamia vema Baraza kwa niaba ya Ofisi ya Makamu wa Rais ili miongozo inayotolewa na Ofisi itekelezwe kwa weledi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amempongeza Mwenyekiti Prof. Esnati Chaggu na wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuongoza Taasisi hiyo yenye jukumu kubwa la kusimamia masuala ya mazingira Nchini.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Mhandisi Esnath Chaggu,ameahidi kufanyia kazi maelekezo ya Waziri na kuishauri serikali katika masuala muhimu ya hifadhi na usimamizi wa mazingira.
0 Comments