Ticker

6/recent/ticker-posts

WANADIASPORA WAHAMASISHWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOBUNIWA KWA AJILI YAO

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago akisaini Kitabu cha Wageni kwenye Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar Es Salaam. Bi. Mwakawago alitembelea benki hiyo kujadili na uongozi kuhusu unazishwaji wa bidhaa mpya kwa ajili ya diaspora na maendeleo ya matumizi ya bidhaa zilizopo kwa wanadiaspora.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa benki ya NMB baada ya kufanya mazungumzo na watumishgi hao.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago akiwa na mmiliki wa Hamidu City Park, Bw. Hamidu Mvungi. Hamidu City Park ni mradi wa nyumba uliopo Kigamboni jijini Dar Es Salaam ambao Kaimu Mkurugenzi ameenda kuuona ili kujiridhisha kwa ajili ya kuwahamasisha wanadiaspora kununua nyumba kwenye mji huo.

Sehemu ya nyumba zinavyoonekana kwenye mji huo.


Post a Comment

0 Comments