Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDALICHAKO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CANADA NCHINI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa Canada ukiongozwa na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamela O’Donell (kulia) walipomtembelea leo Februari 21, 2022 katika Jengo la PSSSF, Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamela O’Donell akieleza jambo wakati walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye UlemavU) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akipitia nyaraka zinaonyesha maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi ya Canada na Tanzania.


Kansela Mkuu, Ushirikiano na Maendeleo, kutoka Ubalozi wa Canada, Bi. Helen Fytche akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) walipomtembelea leo Februari 21, 2022 katika Jengo la PSSSF, Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akionyesha zawadi aliyopewa na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamela O’Donell (kulia) alipomtembelea Februari 21, 2022 katika Jengo la PSSSF, Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika picha ya pamoja na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamela O’Donell (kulia) alipomtembelea Februari 21, 2022 katika Jengo la PSSSF, Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

OWM - KVAW

Post a Comment

0 Comments