Ticker

6/recent/ticker-posts

JERRY SLAA: ENDELEENI KUSIMAMIA KIKAMILIFU MIRADI YA MIUNDOMBINU NCHINI

Mwenyekiti Kamati ya Kuduma ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC), Jerry Slaa akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(Ujenzi), Ludovick Nduhiye, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila na Barakaeli Mmari Mhandisi wa Miradi ya BRT wakati kamati hiyo ilipokagua ujenzi wa mradi wa Usafiri wa Haraka wa Mabasi(BRT) Awamu ya Pili Kariakoo-Mbagala leo jijini Dar es Salaam.
Barakaeli Mmari Mhandisi wa Miradi ya BRT akitoa maelezo kwa Mh. Jerry Slaa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) katikati na wajumbe wake, wa tatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(Ujenzi), Ludovick Nduhiye na wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila
Moja ya Daraja linalojengwa eneo la BP ambapo magari yatapita juu na treni itapita chini katika barabara ya Kilrwa jijini Dar Es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(Ujenzi), Ludovick Nduhiye akimsikilia mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Temeke Mh. Dorothy Kilave alipokuwa akiuliza swali.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo kwa kamati.
........................................................

Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC), Jerry Slaa amesema TANROADS imeendelea kufanya kazi kubwa kwa taifa na kusimamia kikamilifu ujenzi wa miundombinu kwa sababu wamepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Samia Suluhu Hassan kufanya kazi kwa bidii.

Jerry Slaa ameyasema hayo wakati Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, ikipokea taarifa ya mradi wa Usafiri wa Haraka wa Mabasi(BRT) Awamu ya Pili, ambao unasuasua kukamilika tofauti na muda wa ukamilishaji wa mradi huo.

Ameitaka TANROARDS kuendelea kumsimamia kwa ukamilifu mkandarasi anayejenga miundombinu ya barabara ya Usafiri wa Haraka Awamu ya Pili kutoka Gerezani hadi Mbagala ili kuhakikisha serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza azma yake ya kufanya kazi kwa kasi kubwa.

Amebainisha kwamba mradi huo ni muhimu na ndio maana Rais Samia alitoa maagizo ya kutaka mradi kumalizika kwa haraka ili wananchi waweze kunufaika na huduma ya usafiri ya mradi huo, ambao kumalizika kwake utakuwa na faida kubwa.

''TANROADS mnafanya kazi nzuri lakini mwenendo wa makandarasi sio mzuri, mnapaswa kumfuatilia kwa karibu ili amalize mradi huu kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa. Kwa kuwa kuchelewa kwake kunasababisha sintofahamu kwa wananchi,'' amesema Jerry Slaa.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati hiyo, Augustine Vuma, naye aliitaka TANROADS kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi mbalimbali nchini na kuwachukulia hatua wale wanaochelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Katika mradi huo, kazi za ujenzi wa majengo ikiwemo karakana 1, vituo vikuu 2 na vituo mlisho vinne imeshakamilika toka Julai 31, 2021 na sasa sehemu hiyo iko katika muda wa uangalizi wa mwaka mmoja kama mkataba unavyotaka.

TANROADS imeshakaa na mkandarasi na kuzungumza naye, ambaye kuchelewa kwake kulitokana na matatizo ya Uviko-19, hivyo Machi 27, 2023 mradi huo utamalizika.

Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(Ujenzi), Ludovick Nduhiye, alisema ushauri wote ulitolewa na Bunge kupitia kwa Kamati hiyo utafanyiwa kazi ikiwemo kuusimamia mradi huo na kumalizika kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments