Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauniakiongea na Waandishi wa Habari Unguja, Zanzibar Machi 3, 2026 wakati akitoa kauli yaSerikali katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Afrika inayoadhimishwa kila mwakaMachi 3.
PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Na; Mwandishi Wetu, Unguja
Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na mambo mengine imeimarisha zaidi ushirikiano wakimataifa na kutoa mchango mkubwa katika masuala ya kikanda na kimataifa yanayohusumazingira na mabadiliko ya Tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameyasemahayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Unguja, Zanzibar Machi 3, 2026 wakati akitoakauli ya Serikali katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Afrika inayoadhimishwa kila mwakaMachi 3.
Amesema kupitia ushawishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. SamiaSuluhu Hassan katika medani ya kimataifa, Tanzania imepata fursa za kuongoza masualambalimbali ya kikanda ambayo ni pamoja na kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa Wakuuwa Nchi za Afrika - Misheni 300 uliofanyika Januari 27 hadi 28 Januari, 2025 jijini Dar es Salaam.
Pia Tanzania ilifanikiwa kuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati ya Umoja wa Afrika ya Wakuuwa Nchi na Serikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu waRais, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mkutano wa Nane waBaraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA - 8) kuanzia Desemba 2025 hadi Desemba2027.
Amesema Maendeleo na ukuaji wa taifa lolote duniani pamoja na ustawi wa watu wake vimefungamana na hali na ubora wa mazingira. Hali ya mazingira ikiwa imara ukuaji wa uchumina ustawi wa watu pia huwa imara.
“Tarehe 3 Machi ya Kila mwaka, Bara la Afrika huadhimisha Siku ya Mazingira Afrika, siku hiiadhimu iliasisiwa mwaka 2002 na Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika ikiwa ni moja yamaazimio muhimu ya Umoja wa Afrika katika kuhimiza nchi wanachama na Bara la Afrika kutunza na kuhifadhi mazingira,
“Kauli mbiu ya siku hii kwa mwaka huu ni ‘Assuring Sustainable Water Availability and Safe Sanitation Systems to Achieve the Goals of Agenda 2063". Ambayo tafsiri yake ni: "Uhakikawa upatikanaji Endelevu wa Maji na Mifumo Salama ya Usafi wa mazingira ili kufikiaMalengo ya Ajenda 2063,” amesema Mhe. Masauni.
Amesema, kauli mbiu ya siku ya Mazingira kwa Afrika mwaka huu inahusu Uhakika waupatikanaji Endelevu wa Maji na Mifumo Salama ya Usafi wa mazingira kwa maendeleoendelevu inatukumbusha umuhimu wa kutekeleza mipango shirikishi ambapo mtu na taasisi nimuhimu kushiriki ipasavyo kwa faida ya nchi.
“Kwa kutambua uhalisia huu, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kufungamanishakwa vitendo masuala ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu”.
Ameongeza kuwa Dira 2050 imeweka nguzo adhimu inayohusu Uhifadhi wa Mazingira naustahimilivu dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi. Vile vile, Ilani ya CCM imeweka masuala yamazingira na mabadiliko ya Tabianchi kama mojawapo ya masuala muhimu yatakayozingatiwakatika kipindi cha mwaka 2025 – 2030.
Mhe. Masauni amesema Dunia inapitia katika changamoto kuu tatu za Mazingira ambazo ni: Upotevu wa Bioanuai; uchafuzi wa Mazingira kutokana na vyanzo mbalimbali pamoja naMabadiliko ya Tabianchi.
Amesema, uhalisia huu unakumbusha umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kuimarishauhifadhi wa mazingira pamoja na ufumbuzi wa pamoja wa changamoto za mazingira, ni kwamuktadha huu, Tanzania ni nchi mwanachama wa mikataba mbalimbali inayohusu hifadhi nausimamizi wa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauniakiongea na Waandishi wa Habari Unguja, Zanzibar Machi 3, 2026 wakati akitoa kauli yaSerikali katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Afrika inayoadhimishwa kila mwakaMachi 3.
PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS



0 Comments