Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili fursa za mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) mkoani hapa leo. Kushoto ni Olivier Foulonneau kutoka East African Crude Oil Pipiline na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba ambaye bomba hilo litapita kwenye wilaya yake.
Olivier Foulonneau kutoka East African Crude Oil Pipiline akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Habari kutoka Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC ) Beatrice Peter akitoa taarifa ya mradi huo.
Mratibu wa masuala ya uhusiano wa Jamii Shaban Kimaro akichangia jambo kwenye mkutano huo.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge.
Wakuu wa Wilaya ambazo utapita mradi huo, Mhandisi Paskas Muragili (Singida Mjini) na Sophia Kizigo (Mkalama) wakiteta jambo wakati wa mkutano huo.
Neema Mwakatobe kutoka Baraza la Uwezeshaji Tanzania (NEEC) akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na baraza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Mhandisi Paskas Muragili (kulia) wakiwa kwenye mkutano huo.
Mhandisi Mhina Kihondo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya enquiris @ eals.co.tz akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara Mkoa wa Singida, Kitila Katala akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa Redio Standard FM yaSingida James Daud akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mfanyabiashara Mussa Madadi akiuliza swali.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos akiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akiwa kwenye mkutano huo.
Mfanyabiashara Bula Remy akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mfanyabiashara na mkulima Geofrey Kingu akizungumzia fursa zitakazo patikana kupitia mradi huo.
Martha Makoi- Local Content akiungumzia jinsi wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo watakavyofanya kazi kwa kushirikiana wakati wa utekelezaji wamradi huo..
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida akiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki mkutano huo.
**********************
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge amewataka wananchi na wadau mbalimbali kujiandaa ili waweze kupata fursa za kibiashara zinazokuja kutokana na Ujenzi wa Bomba la Mafuta linalotokea Hoima nchini Uganda hadi Chongerehani mkoani Tanga.
Akifungua mkutano wa wadau mkoani hapa leo wa kujadili fursa za mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Dk. Mahenge alisema ni wakati sasa kwa wafanya biashara na makundi mengine kuchangamkia fursa za kibiashara ili kuboresha maisha yao na taifa kwa ujumla.
"Sasa basi kwetu sisi ni kuchangamkia fursa kwani kutakuwa na kambi kubwa hapa kwetu hivyo kutakuwa na mahitaji makubwa ya nyumba za kulala ,vyakula, uuzaji wa vifaa vya ujenzi na mahitaji mengine mbalimbali", alisema Mahenge.
Alisema utaratibu umeelekeza kwamba mdau au mtu yeyote ambaye atahitaji kufanya biashara yoyote kupitia mradi huo hawezi kupata fursa hiyo bila ya kujisajili Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
Aidha Mahenge alisema jambo kubwa ambalo ni la muhimu ni kufanya maandalizi ya kuitana na kujua shughuli ambazo wanahitaji kuzifanya kwenye mradi baada ya kuziona fursa, kuunda vikundi, kubadilika na kuacha tabia ya kufanya kazi kila mtu kivyake badala yake wabadilishane mawazo ya nini wakifanye kutokana na fursa zilizopo kama ufugaji wa kuku, uandikaji wa miradi na nyingine nyingi.
Afisa Habari kutoka Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC ) Beatrice Peter alisema mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima nchini Uganda kwenda kwenye Peninsula ya Chongoleani mkoani Tanga nchini Tanzania una urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo nchini Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.
Alisema bomba hilo litapita katika mikoa nane ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga. Bomba vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.
Peter aliongeza kuwa kwa Mkoa wa Singida bomba hilo linapita kwenye wilaya tatu za Mkalama ,Iramba na Singida Vijijini na katika wilaya hiyo kutajengwa kambi kubwa namba 11 itakayo chukua wafanyakazi zaidi ya 1,000 ambapo itachochea zaidi kuongeza uchumi wa Singida ikiwa Wana Singida watachangamkia fursa hiyo.
Alisema mpaka sasa katika mikoa yote iliyopitiwa na bomba hilo jumla ya Sh.2.5 Bilioni kwenye maeneo ya kipaumbele wananchi wamekwisha lipwa fidia zao ambapo kwa mkoa wa Singida fedha walizolipwa ni Sh.95 Milioni.
Aidha Peter alisema mwezi huu hatua itakayofuata ni timu kutoka TPDC itapita katika mikoa hiyo nane kwa ajili ya kutoa elimu kuhusiana na mikataba mbalimbali ya wafidiwa wa njia ya bomba ambao ni 9,122 kwa mikoa yote ambapo Sh.22 Bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa fidia.
Mhandisi Mhina Kihondo kutoka EWURA ametoa wito kwa wananchi wa Singida kuchangamkia fursa ya kujisajili kwenye kanzidata yao ambayo itawawezesha kufahamika kama kampuni za ndani ili kampuni kubwa zitakazoshiriki kwenye mradi huo ziweze kuwaona na kuwapa fursa ya utekelezaji wa mradi huo.
Kihondo alisema Mkoa wa Singida umekuwa na kasi ndogo ya kujisajili ukilinganisha na mikoa mingine hivyo alitoa mwito kwa wanasingida kuongeza kasi ya kujisajili ili wanufaike na mradi huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara Mkoa wa Singida, Kitila Katala alisema changamoto kubwa iliyosababisha wananchi na wafanyabiashara wengi kuto jisajili EWURA imetokana na uelewa mdogo kwa walengwa ambao walikuwa hawajui jinsi ya kazi hizo zitakavyopatikana kupitia bomba hilo kutokana na kutokuwepo kwa chombo ambacho kilikuwa kikitoa elimu na uhamasishaji zaidi ya kusikia tu kuna fursa za bomba la mafuta.
Mfanyabiashara wa Singida mjini Bula Remy alisema ni kweli bomba hilo litatoa fursa kwa Wana Singida lakini hofu yao ni pale wanapoambiwa ni lazima wasajiliwe kwanza na EWURA hivyo wasije wakapewa masharti magumu na kushindwa kupata fursa hiyo na kujikuta ikichukuliwa na wafanyabiashara wengine wakubwa kutoka nje ya Singida.
0 Comments