Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA KUJIPAMBANUA KIMATAIFA KIDIPLOMASIA NA KIUCHUMI


*************************

Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki imesema Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Tanzania imefanikiwa kufungua milango Duniani kwa Rais kufanya ziara mbalimbali na kutembelewa na Marais wa nchi nyingine ikiwa ni ishara ya uhusiano mzuri.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula ambapo amesema takribani Mikataba 6 yenye thamani ya Trilioni 1.77 na Euro million 425 imesainiwa kutoka kamisheni ya umoja wa Ulaya ambapo fedha hizo zitatumika kuendeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo hususani ujenzi wa miundombinu.

Aidha amesema Ugeni wa viongozi wa mashirika mbalimbali ikiwemo benki ya Afrika pamoja na kusainiwa kwa mikataba ya kiuchumi na kisiasa ni kiashiria cha mafanikio ya mahusiano mazuri ya kimataifa.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Rais amesaidia kwa kiasi kikubwa kuipaisha Tanzania kidiplomasia Duniani na kusaidia kupatikana misaada mbalimbali ikiwemo chanjo ya Covid 19 na fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na Tanzania kuzidi kutambulika na kushika nyadhifa mbalimbali katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo itasaidia kutetea mambo mbalimbali ikiwemo haki za binadamu.

Hata hivyo amesema kuwa ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Tanzania imefanikiwa kuongeza balozi 2 ikiwemo Indonesia hivyo kufikia balozi 45 Duniani na kuanzishwa kwa idara maalumu ya kusimamia diplomasia ya uchumi.

Ameongeza kuwa Serikali imeshatangaza tenda kwenye baadhi ya balozi za kujenga ofisi zake yenyewe na kujenga majengo ya vitega uchumi katikati viwanja vyao kwa manufaa ya nchi.

Hata hivyo amesema wsmeshafanya jitihada mbalimbali za kuitangaza Tanzania kiuwekezaji na kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania ambapo wameshafanya ziara na kuzungumza na taasisi za biashara Duniani hivyo watanzania wachangamkie fursa na wizara inafungua milango kushirikiana na wananchi katika kufikia fursa zilizopo

Post a Comment

0 Comments