Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA KIWANDA CHA GSM KILICHO UNGUA

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akizungumza na baadhi ya viongozi wa GSM mara baada ya kutembelea kiwanda cha GSM kilichoungua hivi karibuni ili kujionea hitirafu iliyotokea. Kiwanda cha GSM kilichoungua hivi karibuniNaibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akiwa na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi zinazosimamiwa na Wizara wakitazama kiwanda cha GSM kilichoungua mara baada ya kutembelea kiwanda hicho. Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha GSM mara baada ya kutembelea kiwanda cha GSM kilichoungua hivi karibuni ili kujionea hitirafu iliyotokea.

****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Serikali imewataka wenye viwanda nchini kuhakikisha wanaweka tahadhari zote ikiwemo za moto na kuendelea kuwa na bima ambayo itawasaidia pindi ikitokea itirafu yoyote kwenye kiwanda na kusababisha kupoteza mali zake waweze kufidiwa mara moja

Ameyasema hayo leo Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe mara baada ya kutembelea kiwanda cha GSM kilichoungua hivi karibuni ili kujionea hitirafu iliyotokea.

Amesema baada ya uchunguzi kukamilika katika kiwanda hicho basi wapo tayari kuwasikiliza GSM kuona ninamna gani Serikali inaweza ikawasaidia ili uzalishaji uweze kuendelea.

"Hili ni pigo sio kwa GSM pekee bali kwa nchi nzima lakini pia kwa Serikali ambayo inapenda viwanda viendelee kuzalisha bidhaa muhimu ambazo zinatumika katika nchi yetu". Amesema

Amesema Serikali inawajibu wa kulea Sekta Binafsi hasa kwenye viwanda ili waendelee kuzalisha kwa tija, kutoa ajira na kuokoa fedha ambazo zingetumika kama bidhaa hizi zinazozalishwa na kiwanda husika zingeagizwa kutoka nje ya nchi.

Kwa upande wa GSM wameshindwa kuzaungumza kwa maana wakisubiri Uchunguzi ufanye na baadae wataeeleza ni nini kifanyike na pia kutoa maoni yao kwa Serikali.

Post a Comment

0 Comments