Ticker

6/recent/ticker-posts

TUNATAKA LISHE BORA SHULENI ILI WATOTO WAKUE VIZURI-RC MJEMA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga. Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Dafroza Ndalichako akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Dafroza Ndalichako(kushoto) akizungumza jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati wa kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga. Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kikao na Mkuu wa Mkoa huo kujadili maendeleo ya elimu na kuboresha elimu mkoani humo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Sophia Mjema amewaagiza Wakuu wa Wilaya wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa Chakula Mashuleni ili kuboresha lishe shuleni kwa Mkoa wa Shinyanga.

Agizo hilo amelitoa leo Tarehe 03/03/2022 wakati akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu na kuboresha elimu mkoani humo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

"Tunataka lishe bora shuleni ili watoto wakue vizuri. Tukasimamie pia mdondoko, watoto wafuatiliwe wako wapi, watoto wanatakiwa wawe shule kama tulivyowaandikisha, tusikubali kuwa chini ya asilimia 100”, Amesema RC Mjema.

Amesema wanachotaka kufanya kwasasa ni kuboresha mazingira ya elimu katika mkoa huo ambapo ameagiza uwepo wa ushirikiano wa kutosha kwa upande wa shule za Serikali na binafsi ili malengo hayo yaweze kutimia kwa ufasaha.

"Tunataka shule zetu ziingie kumi bora kitaifa kila mwaka.Walimu na wadau wote tuwe wabunifu, wakurugenzi tuwe na ubunifu pia kwa kuwapa motisha walimu ikiwemo kuwapatia nyumba, mtaona hawataondoka, hawatakimbia na ufaulu utaongezeka". Amesema

Sambamba na hayo RC Mjema ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria walimu watakaobainika kudai malipo kwa wanafunzi na kusisitiza kuwa Serikali inatoa elimu bure.

"Napenda kusisitiza kuwa elimu ni bure,hakuna malipo, mwalimu yeyote atakayebainika kuchangisha fedha achukuliwe hatua". Ameeleza.

Post a Comment

0 Comments